Nyota wa filamu aliyefariki dunia ghafla juzi Jijini Dar es Salaam, Adam
Philip Kuambinana, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne kwenye makaburi
ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Nyota
wa filamu aliyefariki dunia ghafla jana Jijini Dar es Salaam, Adam
Philip Kuambinana, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne kwenye makaburi
ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Kwa Mujibu wa mratibu wa shughuli hiyo ya mazishi Steve Nyerere, Mwili wa Marehemu Adam Philip Kuambiana utapelekwa viwanja vya Leaders siku hiyo ya Jumanne kwa ajili ya wadau ndugu jamaa na marafiki kuuaga kabla ya maziko.
Marehemu Kuambiana alifarki dunia jana akiwa njiani kuelekea hospitali ya Mama Ngoma Mwenge Dar es Salaam baada ya kuanguka akiwa kwenye upigaji picha filamu katika hoteli moja iliyopo eneo la Sinza.
Inadaiwa kabla ya umauti kumfika marehemu alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo.
Enewz inatoa pole kwa familia ya marehemu na Mungu ailaze roho ya Marehemu Adam Kuambiana mahali pema peponi Amina.






Dar+Es+Salaam
0 comments:
Post a Comment