Monday, May 19, 2014

Genevieve Nnaji :naogopa kuolewa

Nyota wa filamu nchini Nigeria Genevieve Nnaji ameweka wazi kuwa hayuko tayari kuolewa kwa sasa kwa kuwa hajaona mtu anayestaili kuolewa naye.

                                         GENEVIEVE NNAJI
Wanawake wengi wamekuwa na mitazamo tofauti likija suala la kuchagua wenzi wao wa Maisha. Hali hiyo haitofautiani sana kwa mwanadada nyota wa Nollywood Genevieve Nnaji ambaye ameweka wazi kuwa, limekuwa si suala rahisi kwa yeye kutafuta mwenza.
Nyota huyu ambaye ni mama wa mwanadada mwenye umri wa miaka 18 anasema kuwa katika maisha yake hajampata mtu ambaye anadhani wanaendana kiasi cha kuwa tayari kumsamehe kwa lolote iwapo atakosea.
Genevieve mwenye umri wa miaka 34 hivi sasa ni kati ya wasichana wengi nchini Nigeria waliopata ujauzito wakiwa na umri mdogo wa miaka 16 tu, japo alifanikiwa kumuweka mtoto wake mbali na mapaparazzi mpaka hivi karibuni, huenda ni kwa sababu mtoto wake huyu anaishi na baba yake barani Ulaya.
Genevieve anasema sio siri wanawake wengi wanatamani ndoa lakini kupata wenza sahihi ndiyo changamoto kubwa, na kuongeza kuwa licha ya kuwahi kuchumbiwa mara kadhaa ikija suala la kuoana anakua muoga sana.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...