Msanii wa nchini Rwanda, Aisha Uwimana maarufu zaidi kama Ciney
ameendelea kupiga hatua katika muziki wake na safari hii amefanikiwa
kupata shavu la mkataba wa miaka mitatu chini ya Record Label kubwa
ambayo inakwenda kwa jina Infinity.
Msanii
huyu tayari amekwishafanya rekodi 3 chini ya lebo hii, huku akiwaahidi
mashabiki zake kazi nyingine kali zikiwemo kolabo na wasanii wakubwa
wanaofanya vizuri katika game ya muziki Rwanda.
Ciney amejijengea umaarufu mkubwa kupitia kazi yake inayokwenda kwa jina Game of Love, akiwa amejipanga kuachia video ya kazi yake ya kwanza chini ya Infinity, ya rekodi yake mpya inayokwenda kwa jina Salam.

No comments:
Post a Comment