Sunday, May 18, 2014

wagosi wa kaya waja na msaga sumu

Wagosi Wa Kaya wampa shavu
Ujio mpya wa Wagosi wa Kaya unaonekana sio wa kutabirika kirahisi kwa kuwa hauwezi kujua watapiga hatua gani kutokana na surprises za watu mbalimbali wanaowashirikisha kwenye project yao mpya ya UAMSHO.
Majina ya wasanii wakubwa kwenye game kama Lady Jay Dee, Profesa Jay, Roma na Juma Nature ni miongoni mwa wasanii watakaosikika kwenye albam ya UAMSHO.
Lakini, sio hao tu na wala usiwaze upande mmoja tu…. Wagosi Wa Kaya wamemnasa mfalme wa ngoma na ladha za Uswazi maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’.
Wagosi wa Kaya tayari wamesharekodi wimbo na ‘Msaga Sumu’ kwenye studio za Kama Kawa na ngoma wameibatiza jina la ‘Misala’.
“Moja ya sababu kubwa ya kumshirikisha Msaga Sumu ni kwa sababu yeye ni mtoto wa Uswazi anaejulikana sana na anaushawishi mkubwa kwa watu wake na sisi tunahitaji kuwafikia pia watu hao kwa sababu kazi ya sanaa tunayoifanya sisi hatubagui. Ilimradi kuwe na ujumbe na burudani.” Mkoloni kafunguka
Amesema wimbo waliofanya na Msaga Sumu ni wimbo wenye ujumbe halisi wa mazingira ya Uswazi ambako vijana wengi hukutwa na Misala tofauti na vijana wanaoishi kwenye ngome za kishua.
Unamkumbuka msaga sumu? Kama uko Mkoani, huyu ndiye mfalme wa Uswazi ambaye alipata nafasi ya kutoa tuzo moja ya KTMA 2014. Ni maarufu  zaidi katika kuchombeza maneno kwenye nyimbo za miduara, mchiriku, mnanda na taarabu, “Nampenda Simba/Yanga Shabiki wa Damu.” Ni neno alilolipa umaarufu yeye.

No comments:

Post a Comment