Monday, May 19, 2014

Frank Lampard kumsaidia Steven Gerrard kukiongoza kikosi cha Uingereza huko Brazil

Frank Lampard kumsaidia Steven Gerrard kukiongoza kikosi cha Uingereza huko Brazil
Kiungo wa klabu ya Chelsea Frank Lampard, amekabidhiwa jukumu la kuwa nahodha msaidizi wa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza, ambacho kitakwenda nchini Brazil kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka huu.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson, amemtaja kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35, kwa kuamini uwezo na ujasiri alionao uwanjani ni kigezo tosha cha kuwa msaidizi wa kiungo wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard.
Sifa nyingine ambayo imetajwa na kocha mkuu Roy Hodgson, ya kumtangAza Frank Lampard kuwa msaizidi wa Steven Gerrard ni uzoefu alionao wa kuitumikia timu ya taifa ambapo mpaka sasa ameshacheza katika michezo 103.
"Frank atakuwa msaidizi wa Steven, na ninaamini nafasi hii inamfaa kutokana na ujuzi mkubwa na maafira aliyonayo kwa sasa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.”
"Ninahakika uteuzi huu ni sahihi kwangu na kwa wengine pia, kutokana na ushauri ambao nimeufanyia kazi kutoka kwa wahusika katika benchi langu la ufundi.”
"Ninatarajia Frank Lampard atafanya kazi yake ipasavyo pale, Steven Gerrard atakapokuwa nje ya uwanja kwa sababu mbali mbali, na uhodari wake wa kuwa kiongozi utakuwa kilelezo kizuri kwa wachezaji wenzake.” Amesema Roy Hodgson
Timu ya taifa ya Uingereza itaanza maandalizi ya kuelekea nchini Brazil juma hili, na inatarajiwa kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Peru, Ecuador pamoja na Honduras kabla ya mchezo wake wa kwanza wa fainali za kombe la dunia kwa kuikabili timu ya taifa ya Italia, June 14.
Timu ya taifa ya Uingereza imepangwa katika kundi la nne, sambamba na Italia, Uruguay pamoja na Costa Rica.

No comments:

Post a Comment