Tukio la ajali ya gari ambalo limeripotiwa kumhusisha msanii Bebe Cool
katika barabara ya Entebbe, limetajwa kuwa ni mpango ambao umetengenezwa
kwaajili ya kuvuta watu katika onyesho la “Best of Bebe Cool”
litakalofanyika hivi karibuni.
Kwa
mujibu wa wachunguzi wa mambo, timu ya Bebe Cool imekuwa ikipanga tukio
hili sambamba na mengine kadhaa kwa mwezi mzima, mpango ukiwa ni
kutangaza kuwa staa huyu amepoteza fahamu na baadaye kuja kuzinduka siku
chache kabla ya show.
Hakuna majibu yoyote kutoka kambi ya Bebe Cool mpaka sasa kwaajili ya kutoa ufafanuzi wa swala hili, na rekodi inaonyesha kuwa ni kweli wasanii wa Uganda wamekuwa na utaratibu wa kutengeneza matukio ili kuvuta mashabiki kufuatilia wanachokifanya.

0 comments:
Post a Comment