Wednesday, June 25, 2014

Tunadharaulika wasanii wa vichekesho-Mboto

Msanii wa vichekesho Tanzania, Mboto Haji maarufu kama Mboto amesema kuwa fani ya uigizaji wa vichekesho imekuwa ikidharaulika sana na watu kiasi hata cha kufanya baadhi ya wasanii wa vichekesho nchini kushindwa kujiamini na

                                     Msanii wa vichekesho Mboto Haji akichat
kufanya kazi kwa kipato cha chini kutokana na fani hiyo kudharaulika,Mboto amesema.
Mboto ameweka wazi kuwa hata yeye mwanzo alikuwa akidharaulika na hata alipokuwa akitoa mawazo kwa wadau ili awezekufanya jambo fulani wadau hao walimpuuza na kuona kuwa kitu kama hicho akiwezekana,lakini kwa kuweka nia na malengo aliweza kufanya jambo ambalo liliweza kumpandisha na kupandisha heshima yake kiasi cha watu waliokataa kufanya nae kazi awali walirudi na kuhitaji kufanya naekazi tena kwa kumlipa pesa za chini,lakini kwa kuwa anatambua nini anafanya aliwahitaji kujiongeza na kumlipa pesa anayohitaji.
ASILI YANGU NA JINA MBOTO
Mboto amefunguka na kusema kuwa kwa asili yeye ni mtu wa pwani yaani ni Mzaramo na jina lake analolitumia katika tasnia ya uchekeshaji alipewa na msaniii Max ambaye kwa sasa ni marehemu.
NIMEPATA VINGI KUPITIA SANAA
Mkali huyu wa uchekeshaji katika kiwanda cha filamu amedai kuwa fani yake hiyo ya uchekeshaji imemfunza mambo mengi na kumsaidia kufanya mambo mengi ambayo awali alikuwa akiona kama ndoto lakini kupitia fani hiyo ameweza kufanya ndoto kuwa kweli.anadai mbali na kufahamika lakini pia kazi hiyo ndiyo inamfanya aendeshe maisha yake hapa mjini lakini pia anakili wazi kuwa kazi hiyo ndiyo imeweza kumfanya kupata au kufanya biashara aliyokuwa akiitamnai kuifanya siku zote.
"Kupitia sanaa hii hii ya uchekeshaji nimeweza kupata biashara ambayo niliokuwa nikiiwaza sana katika maisha yangu"
WASANII NAO WAKUBALI NYUMBANI
Mboto amedai kuwa katika kufanya kazi na wasaniii mbalimbali na kuangalia kazi zao pia kuna wasanii wawili ambao yeye anawakubali na kuheshimu kazi zao sanaa ambao ni Kigwendu Kingwendulile pamoja na msanii Aunty Ezekil hao ni katika tasnia yao ya uigizaji lakini kwa upande wa msaniii wa bongo fleva anamkubali sana Msanii Juma Kassim Nature 'Kiroboto'
MBALI NA SANAA NINGEKUWA ASKARI
Mboto amesema kuwa kama ingetokea asingekuwa katika tasnia ya uigizaji basi angetamani sana kuwa polisi wa Tanzania maana ni moja ya kazi ambazo alikuwa akizitamani kuzifanya toka kitambo.
"Kama nisingekuwa mchekeshaji au msanii wa filamu hakika ningetaman kuwa askari kwenye jeshi la la police Tanzania maana ni kazi niliyokuwa naipenda sana".
Mboto amesema kwa sasa anajiandaa kufanya kazi nyingine ambayo anaimani itakuja kufanya vizuri pindi itakapotoka.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...