Studio za Noiz Makah chini ya Producer DX, zimetoa mixtape ya midundo
ya hip hop 10 waliyoipa jina la Biashara Ngumu Volume 1, wanayoigawa
bure kwa msanii yeyote wa Hip Hop.
DX aliiambia THADE EXPENSIVE kuwa jina la mixtape
hiyo, ‘Biashara Ngumu’ linatokana na aina ya midundo iliyomo ambapo
midundo mitano ni ya Hip Hop biashara (laini) na mitano mingine ni Hip
Hop ngumu.
Akieleza kuhusu lengo la kuitoa mixtape hiyo, DX amesema kuwa ni kusapoti wasanii hasa wachanga.
“Nia ya projet yenyewe ni kuweza kusapoti wasanii especially wasanii
chipukizi kwa sababu kwenye tasnia ya muziki especially category ya Hip
Hop tuna wasanii wengi chipukizi wanataka kuonesha ujuzi wao kupitia
talent shows, kupitia hizi open stage/open mic na hat offer wanazopewa
katika studio mbalimbali hapa Tanzania. Sasa sisi kama Noiz Mekah
tumeona ni vizuri kusapoti.”
Ameeleza kuwa beat hizo zitaendelea kutoka kama mixtape na hiyo ni
Volume 1, kwa hiyo zinakuja nyingine zaidi na zinapatikana bure kupitia
website ya mkito.com.
0 comments:
Post a Comment