Sunday, July 13, 2014

Katika Histoaria: Mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la dunia mwaka 2014

Katika Histoaria: Mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 Argentina itakuwa inakutana na Ujerumani kwa mara ya tatu katika mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la dunia ambayo ni rekodi mpya baina ya mahasimu hao wawili.
Mbali na mchezo wa hatua ya fainali, mafahari hao wawili kwa mwaka 2014, pia wamewahi kukutana mara 5 katika michezo ya hatua tofauti ya michuano hiyo mikubwa duniani.
Mwaka 1958 (Sweden)
Wajerumani wakiwa ndio mabingwa watetezi wa kombe la dunia, waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhdii ya Argentina katika mchezo wa hatua ya makundi.

Mwaka 1966 (Uingereza)
Ujerumani walitoka sare tasa na Argentina katika mchezo wa hatua ya makundi.

Mwaka 1986 (Mexico)
Argentina waliibuka washindi kwa mabao 3-2 dhidi ya Argentina katika mchezo wa hatua ya fainali.

Mwaka 1990 (Italia)
UJerumani waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Argentina baada ya kupata penati katika dakika ya 85.

Mwaka 2006 (Ujerumani)
Ujerumani waliitoa Argentia kwa changamoto ya mikwaju ya penati (4-2) katika mchezo wa hatua ya robo fainali baada ya timu hizo kwenda sare ya kufungana bao moja kwa moja katika muda wa dakika 120.

Mwaka 2010 (Afrika Kusini)
Ujerumani waliifunga Argentina mabao manne kwa sifuri katika mchezo wa hatua ya robo fainali.
Argentina ilikuwa ikinolewa na Diego Maradona.
Swali linakuja.
Je, ni nani ataibuka kidedea leo?
*Muhumu: Nchi zilizo kwenye mabano ni wenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka huo.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...