Msanii maarufu wa kike raia Sweden mjini Stockholm mwenye makazi yake
nchini Tanzania, Saraha amerudi nchini kwa ajili ya maandalizi ya
kurekodi nyimbo na kushoot videos zake mpya.
Saraha
ameongea na thade expensive kuwa anatarajia kuchukua muda usiopungua mwezi mmoja
na nusu kufanya kazi hizo nchini, ambapo ameweka wazi kuwa wiki ijayo
atatoa wimbo wake mpya alioubatiza jina 'Shemeji' ambao umetengenezwa
nchini Sweden na prodyuza anayeitwa Memo Crecendo.
Mwanadada huyo ameongezea kuwa wakati wimbo huo ukiwa hewani anafanya maandalizi pia ya "kushoot" video ya wimbo huo nchini Tanzania chini ya kampuni ya Dream Production na kuongozwa na Raymond Kasoga.
Aidha, Saraha aliyepotea kwa kipindi kirefu nje ya nchi amesema kuwa atarudi tena nchini Sweden kumalizia masomo yake huku nyimbo zake nyingi zikipigwa katika vituo mbalimbali nchini humo ukiwemo wa 'Mbele Kiza' .

0 comments:
Post a Comment