Historia mpya imeandikwa kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya nane bora
iliyozikutanisha Uholanzi dhidi ya timu ya Costa Rica, ambayo kwa mara
ya kwanza imefanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya kombe la dunia.
Mchezo huo uliomalizika hivi punde umetumia zaidi ya dakika 120 ili
kuamua timu ya kwenda kuchuana na Argentina kwenye nusu fainali.
Dakika 90 za mchezo huo ziliisha kwa matokeo ya sare tasa, na mpaka
mpira unakwenda dakika 30 za nyongeza na kumalizika milango bado ikabaki
migumu na ikaamuliwa kwenda kwenye mikwaju ya penati.
Uholanzi ikiwa haijawahi kushinda kwenye mikwaju ya penati katika
mashindano ya kombe la dunia, ikafanikiwa kushinda kwa penati 4-2 dhidi
ya Costa Rica.
Pia hii ni mara ya kwanza kwa Uholanzi kushinda mechi yoyote ambayo imevuka kwenda kwenye hatua ya dakika za nyongeza.
Kwa matokeo hayo sasa Argentina itakutana na Holland jumatano usiku, wakati Brazil ikukutana na Ujerumani jumatatu hii.
0 comments:
Post a Comment