Bajeti kubwa aliyokuwa anaitaja Shetta katika video ya wimbo wake wa
‘Kerewa’ imeanza kuzaa matunda baada ya video hiyo kuanza kuoeneshwa na
kituo cha MTV Base.
Shetta haujutii ushauri aliopewa na Diamond kutumia kiasi cha Milioni
takriba 30 za kitanzania kuhakikisha mzigo unatoka vizuri na kwa
kiwangu cha juu.
Hii ni hatua kubwa kwa msanii huyo kwa kuwa inakuwa video yake ya kwanza
kuanza kuonekana katika channel hiyo ya kimataifa na bila shaka matunda
zaidi yanakuja.
0 comments:
Post a Comment