Thursday, July 3, 2014

Grand Pa Records yaeleza sababu za kuondoka kwa DNA katika label hiyo

Grand Pa Records yaeleza sababu za kuondoka kwa DNA katika label hiyo

Baada ya rapper DNA kutoka nchini Kenya kutangaza kuachana na Lebel iliokuwa inamsimamia Grandpa Records akidai anataka kufanya kazi zake kwa kujitegemea lebel hiyo imetoa tamko kuhusu kilicho sababisha jamaa kuondoka
Grand Pa Records iliyokuwa familia ya rapper DNA ilitangaza kuachana na rapper huyo hali iliyozua maswali na gumzo mitaani na kwenye media.
Baada ya maelezo mengi kuzunguka kwenye mitandao, DNA alifanya mahojiano na kituo cha radio cha Citizen radio na kueleza kuwa aliamua kuachana na label hiyo kwa hiari yake bila kuwepo ugomvi na kwamba lengo ni kutaka kuwa msanii anaejitegemea ili akamilishe mipango yake.
Grand Pa Records nao wametoa tamko rasmi linaloeleza sababu za kuondoka kwa DNA na kusafisha anga juu ya tetesi zote zilizokuwa zinaendelea.
"GrandPa Records/GrandPa Government imekuwa ikikuwa na kusimamia wasanii wenye majina barani africa,DNA alikuwa nisehemu ya familia yetu ,tumehusika kwenye mafanikio yake makubwa baada ya kurudi kwenye game mafanikio ambayo hayajawi kutokea katika msanii wa afrika mashariki na tumekuwa pamoja katika miaka miwili ambayo tumefanya kazi pamoja ,ni msanii mwenye kipaji.
mkataba wake na  Grandpa Records umeisha may 2014 kwa makubaliano ya pande zote mkataba wake hauto ongezwa na amemaliza mkataba wake vizuri hakuna tofauti kati yake na Grandpa records. GrandPa Records, wasanii ,producers na wafanyakazi wote tunamtakia heri Dennis Waweru Kaggia a.k.a DNA katika kazi zake.”
Tamko hilo linaeleza kuwa Grandpa Records itaachia nyimbo za DNA zilizobakia kwa makubaliano kati yeo na DNA.
Uhusiano wa Grand Pa Records ulionekana kuwa imara kwa kuwa wiki iliyopita alikwua best man kwenye sherehe za kufunga ndoa ya mmiliki wa Grand Pa Records.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...