Friday, August 22, 2014

Ushauri wa madaktari kwa wizara ya afya


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Dkt Seif Rashid
Madaktari wa magonjwa ya binadamu, wameishauri wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhakikisha inapanua wigo wa uboreshaji wa huduma za maabara ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi.
Akizungumza katika majadiliano ya madaktari wa mkoa wa Arusha mtaalamu wa magonjwa ya kina mama Dkt. Frank Msuya amesema wananchi wengi hususani wa kipato cha chini wamekuwa wakikosa tiba sahihi kutokana na kukosa vipimo vya uhakika vinavyoonesha ugonjwa.
Kwa upande wake mtaalamu wa maabara kutoka maabara ya Lancet iliyozinduliwa hivi karibuni jijini Arusha Bw. Ahmed Calleb amesema siku zote utendaji kazi bora wa daktari unafanikishwa na majibu sahihi ya vipimo vya mgonjwa.
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...