Baada ya kulazimishwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja
dhidi ya Leicester City, mashabiki wa klabu ya Arsenal wamembwatukia
meneja wa kikosi chao Arsene Wenger na kumuita dikteta.
Wakizungumza kwa hasira mara baada ya mchezo huo ambao uliunguruma mjini Leicester katika uwanja wa King Power mashabiki hao wamesema, Arsene wenger amekuwa na sababu za makusudi kuiona klabu yao inafanya vibaya huku akitambua fika kinachosumbua kikosini.
Wasema yeye kama meneja siku zote amekua anahisi ndie mtu pekee anaijua sana Arsenal na wala hafikirii kama kuna watu wengine wanaumizwa na kinachotokea uwanjani.
Mmoja wa mashabiki hao amesema ilimuumiza sana kuona mchezo na matokeo yaliyopatikana na ilifikia hatua alijilaumu kwa nini alisafiri kutoka jijini London kuelekea mjini Leicester kwa ajili ya kuishangilia timu yake.
Amesema endapo mzee huyo kutoka nchini Ufaransa atashindwa kubadilika kuna hatari kubwa ya kuendelea kufanya vibaya na mwisho wa yote watashindwa kupambana na timu kubwa kama Chelsea, Man City, Liverpool pamoja na Man utd.
Shabiki mwingine alionyesha hisia zake kwa kusema haiwezekani kila msimu mtu mmoja kuwaumiza kwa kushindwa kufanya maamuzi ya kuwasajili wachezaji ambao wataweza kuleta changamoto mpya na mwishowe wafikie mafanikio kama ilivyo kwa klabu nyingine.
Amesema Arsene Wenger hastahili kufanya kazi kubwa zaidi ya kufanya usajili wa mchezaji anaecheza nafasi ya ushambuliaji pamoja na kiungo mkabaji.
Kwa matokeo ya jana ya sare ya bao moja kwa moja yanaiacha Arsenal ikiwa na point tano huku ikitarajia kupambana na Man City katika mchezo ujao mnamo Septemba 13.

0 comments:
Post a Comment