Fifa imedai kutomtambua Chris Giwa kama rais wa NFF.
Nigeria watafungiwa kushiriki soka la kimataifa siku ya Jumatatu
ikiwa Chris Giwa hatojiuzulu kama rais wa shirikisho la soka nchini
humo.Bodi hiyo inayosimamia soka ulimwenguni imetoa agizo linalodai kuwa halitambui uchaguzi wa Agosti 26.
Adhabu hiyo itaondolewa endapo bodi ya NFF ambayo iliondolewa Agosti 25 ikiwa na Amimu Maigari kama raia, itaruhusiwa kurejea ofisini na kuendelea na kazi.
Uchaguzi mwingine mpya wa kamati ya NFF lazima ufanyike haraka iwezekanavyo.
Tarehe ya mwisho ilitolewa na kamati ya dharura ya Fifa siku ya Jumatano baada ya tarehe 1 Septemba kupita bila Giwa kujiuzulu.

Aliyekuwa rais wa NFF Amimu Maigari ambaye aliondolewa kwa agizo la mahakama.
Kama adhabu hiyo itapitishwa siku ya Jumatatu ina maana mabingwa hao
wa Afrika hawatoweza kucheza mechi ya kufudhu kwa Kombe la Mataifa Huru
Afrika Sepemba 10 nchini Afrika Kusini.Nalo Shirikisho la soka la Afrika limesema kama Super Eagles wataikosa mechi hiyo wataondolewa kwenye mechi za kufudhu.
Nigeria walifungiwa kucheza soka la kimataifa kwa siku tisa mwezi Julai baada ya serikali kuingilia masuala ya shirikisho la soka nchini humo na kumlazimisha Maigari kuachia ngazi kwa maagizo ya mahakama.
0 comments:
Post a Comment