Thursday, September 4, 2014

UN: Dola milioni 600 zinahitajika kupambana na Ebola

UN: Dola milioni 600 zinahitajika kupambana na EbolaUmoja wa Mataifa umetangaza kuwa, ili uweze kuzisaidia nchi zinazotaabika hivi sasa kutokana na kukumbwa na maradhi ya Ebola, unahitajia bajeti ya dola milioni 600. Dakta David Nabarro, Mratibu Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba, UN inafanya juhudi za kukabiliana na virusi vya homa ya Ebola lakini inahitajia kiasi cha dola milioni 600 ili iweze kudhibiti virusi hivyo katika nchi za magharibi mwa Afrika.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Umoja wa Afrika (AU) umetangaza kuwa, wiki ijayo utaitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kukabiliana na kasi ya kuenea virusi vya homa ya Ebola barani humo. Taarifa ya AU imesema, katika kikao hicho kutajadiliwa njia za kuzuia kuenea virusi vya Ebola.  Hadi sasa virusi vya ugonjwa huo vimeripotiwa katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea, Nigeria, Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo zaidi ya watu 1,500 wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...