Rapa mkali kabisa wa muziki wa Dansi Nchini, Mao Santiago baada ya
ukimya wa muda mrefu sasa, eNewz imeweza kukutana na kuzungumza naye
ambapo ameanika mipango yake ya kurejea na kazi mbili kwa mpigo mwishoni
mwa mwezi huu.
Mao Santiago
Mao
Santiago aambaye tetesi zimekuwa zikienea mtaani kuwa matumizi ya dawa
za kulevya ndiyo yamemuweka kando na muziki amesema kuwa, yeye yupo
vizuri tu na kwa sasa anafanya kazi mwenyewe akiwa anatumia nafasi hii
kupumzisha kichwa chake kabla ya kurejea tena kwa kishindo katika
muziki.
Repa huyu hata hivyo ameweka wazi kuwa, yupo tayari kufanya kazi na Bendi yoyote ambayo itakuwa tayari kufanya naye kazi bila siasa nyingi.
Repa huyu hata hivyo ameweka wazi kuwa, yupo tayari kufanya kazi na Bendi yoyote ambayo itakuwa tayari kufanya naye kazi bila siasa nyingi.
0 comments:
Post a Comment