Msanii wa miondoko ya Bongo Bolingo Flava, H Baba anaweza
kuwa msanii wa kwanza mkubwa Tanzania kujitokeza hadharani kutaja
kiwango kidogo zaidi alichotumia kushuti video ya wimbo wake.
Bila kung’ata neno wala kuongeza sifuri, H Baba alieleza kuwa video ya wimbo wake
mpya Tubebane aliofanya na muongozaji kutoka Mwanza ‘Saimaco’ ilimgarimu
kiasi cha fedha za Kitanzania 150,000 tu.
“Unajua watu wengi wanaweza kukwambia ‘H Baba hatumuoni…’ waangalie
video yangu niliyoshuti kwa 150,000 tu. Haina sifuri mbele. Ni laki na
nusu na video inaitwa Tubebane. Ni bonge la video…”Alisema H Baba.
“Unajua sisi wasanii tusipende kuongea uongo kwa sababu uongo unaweza
kutuletea matatizo. Matatizo ni yapi, mashabiki wanajua sisi tuna pesa
kumbe pesa hatuna.” Aliongeza.Ameeleza kuwa bei hiyo imetokana na ofa aliyopewa na Saimaco kushuti
video hiyo bure kabisa na gharama alizoingia ni kulipia chakula kwa watu
waliohusika kukamilisha zoezi hilo na mafuta ya gari.
0 comments:
Post a Comment