Jana dunia ilikumbuka tukio kubwa na baya la kigaidi lilolofanywa na
kundi la Al Qaeda chini ya uongozi wa Osama Bin Laden mwaka 2001 baada
ya kushambulia majengo ya kitengo cha ulinzi cha Marekani jijini
Washington na jengo la biashara huko New York na kuuawa takribani watu
3,000.
Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kufuatia vitendo vya kigaidi
vinavyozidi kushamiri katika ukanda wa Afrika hususani kundi la
Alshabaab linalofanya mashambulizi ya kushitukiza katika nchi jirani ya
Kenya.
Hayo yamesemwa na mnadhimu wa kikosi cha usalama barabarani (SACP),
Johansen Kahatano .
Kahatano ameeleza kuwa hivi sasa kundi la Alshabaab lipo katika
harakati ya kulipiza kisasi kufuatia kuuawa kwa kiongozi wao na majeshi
ya Marekani hivyo raia wanapaswa kuwa makini na kutoa taarifa mara moja
polisi pale wanapomtilia mashaka mtu yeyote.
“Nitoe wito tu kwa wananchi kwamba tuchukue tahadhari ya kutosha sisi
wenyewe kwa maana ya kutaka kujilinda dhidi ya jamii inayotuzunguka.
Unapokuwa na mashaka na mtu ambaye hafahamiki sawasawa, awe amebeka kitu
ambacho kinatia shaka. Hasa kwenye mabasi pale unamuona mtu anasafiri
na mzigo wake halafu anashuka anauacha pale kwenye basi. Hata katika
mikusanyiko ya watu wengi, ukishakuwa na mashaka na mtu lazima taarifa
itolewe kwa askari.” Ameeleza.
Kuhusu September 11, 2001:
Ilikuwa siku ya Jumanne, September 11 mwaka 2001 ambapo kundi la
kigaidi la Al Qaeda chini ya uongozi wa Osama bin Laden liliteka ndege
za Marekani, American Airlines Flight 11 na United Airlines Flight 175
na kuzigongesha kwenye matawi ya Kusini na Kaskazini ya jengo la ulinzi
la Pentagon, Washington na Jengo la Biashra ‘World Trade Center Complex’
huko New York.
Ndege nyingine zilizotekwa haziweza kutekeleza shambulizi na kulipuka
wakati abiria walipokuwa wanafanya jitihada za kujiokoa mikononi mwa
watekaji.
Watu takribani 3,000 walipoteza maisha na kusababisha hasara ya zaidi ya takribani $ billion 10.
Osama Bin Laden alithibisha kuwa kundi hilo ndilo lililotekeleza
tukio hilo japo alikanusha kuhusika na tukio la shambulizi la balozi za
Marekani nchini Tanzania na Kenya..
Osama alitaja sababu za kutekeleza tukio hilo kuwa ni uwepo wa vikosi
vya Marekani nchini Saudi Arabia na vikwazo ilivyowekewa nchi ya Iraq
na sapoti ya Marekani kwa Israel katika vita ya ukanda wa Gaza.
Shambulio la September 11 lilikuwa shambulio baya la kigaidi katika
historia ya Marekani ambapo maafisa wengi zaidi na raia walipoteza
maisha.
Marekani ilianzisha mashambulizi makali nchini Afghanistan wakimsaka
Osama Bin Laden na vikundi vya Taliban vilivyokuwa vimemficha.
Vikosi vya Marekani vilimuua Osama bin Laden mwaka 2011 nchini Pakstani baada ya msako wa miaka 10.
0 comments:
Post a Comment