Msanii
'YP' toka kundi la TMK Wanaume Family amefariki dunia jana usiku katika
hospitali ya Temeke ambako alikuwa akipatiwa matibabu akisumbiliwa na kifua kwa muda mrefu
lakini hali ilikuwa mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.
Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fela amethibitisha kutokea kwa msiba
huo. Msiba wa msanii huyo uko Keko nyumbani kwa baba yake.
Said Fella amesema Marehemu ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambikile
alifanya vizuri na msanii mwingine Y Dash na nyimbo kama 'Ulipenda
Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama
'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi'
na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family.
0 comments:
Post a Comment