Kituo kipya cha daladala cha Ubungo
kilichohamishiwa Kituo cha Simu, kati ya barabara ya Sam Nujoma na Sinza
jijini Dar es Salaam, kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho kutwa
(Alhamisi).
Kwa mujibu wa
taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),
Daladala zinazotoka Masaki zikifika barabara ya Shekilango zitaingia
kulia kwa kutumia barabara ya Tanesco inayokwenda moja kwa moja kituoni
Simu 2000 na zitarudi barabara ya Shekilango kwa kutumia njia hiyo hiyo
ya Tanesco.
Zinazotoka Kariakoo, Posta na Kariakoo zikifika
mataa ya Ubungo zitaingia kulia (barabara ya Sam Nujoma) kwenda kituoni
Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.
Aidha, kwa daladala zinazotokea barabara ya Mandela, madereva wake
wameelekezwa; Kuvuka mataa ya Ubungo (kwa kutumia barabara ya Sam
Nujuma) na kwenda kituoni Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia
barabara hiyo hiyo.
Zinazotoka Mwenge zikikaribia Jengo la
Mawasiliano Towers zitachepukia kushoto kwa kutumia barabara ya akiba
inayopita mbele ya Mawasiliano Towers hadi kituoni Simu 2000, zitarejea
zilikotoka kwa kutumia barabara ya Sam Nujoma.
Na zile
zinazotoka Kimara na Mbezi, zikifika mataa ya Ubungo zitaingia kulia
kwenda kituoni Simu 2000. zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo
hiyo.
0 comments:
Post a Comment