Wikendi iliyopita Brad Pitt aliingiza filamu mpya sokoni inayoitwa
Fury, filamu aliyoigiza maisha magumu ya mapambano ya kijeshi wakati wa
vita ya pili ya dunia.
Ubora wa ‘Fury’ uliiwezesha kushika nafasi ya kwanza kwenye chart ya
filamu ‘Box Office’ na kuiondoa ‘Gone Girls’ iliyokuwa ikishikilia
nafasi hiyo.
Ingawa filamu hiyo haihusiani kabisa na masuala ya kifamilia lakini
uhusika wa uongozi wa kikosi cha jeshi kilichokabiliwa na mateso ya
baridi kali, njaa na maafa wakati wa vita ya pili ya dunia umemfanya
Brad Pitt kuwa baba bora zaidi kwa watoto wake sita na mkwewe Angelina
Jolie.
“Uhusika huu ni somo halisi katika uongozi na kujifunza kutaka
heshima na kwa sababu hiyo, hivi sasa ni baba bora zaidi,” Brad Pitt
aliwaambia waandishi wa habari.
0 comments:
Post a Comment