Wakati akiandamwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuvaa sare
za jeshi hilo bila ruhusa maalumu, msanii wa muziki wa kipya nchini,
Naseeb Abdul maarufu kama Diamond amepigiwa chapuo na mtangazaji wa
kituo cha Channel O, Jokate Mwegelo.
Mwegelo amewataka Watanzania kumpigia kura Diamond katika shindano la
tuzo ya video bora Afrika inayofanyika nchini Afrika Kusini.
Alisema Watanzania wanatakiwa kuweka uzalendo mbele kwa kumpigia kura
msanii huyo kwani ushindi wake utaisaidia Tanzania kuzidi kujulikana
kimataifa katika sekta ya muziki na hata katika masuala mengine ya
utamaduni.
0 comments:
Post a Comment