Baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva wakiimba kwa pamoja.
Semina maalumu ya wasanii mbalimbali iliyoandaliwa na Kamati ya Siku
ya Msanii inafanyika kesho Alhamisi katika Ukumbi wa Makumbusho ‘Mwalimu
Nyerere’ Posta jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari , Ofisa Uhusiano wa Siku ya Msanii, Petter Mwendapole, alisema maandalizi yote kwa ajili ya semina hiyo yamekamilika na wasanii 400 hadi kufikia jana wamejiandikisha.

Wasanii wkiadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Alisema lengo ni kuwaelimisha wasanii katika kazi zao, lakini pia
kuwapa nafasi ya kupata mafunzo yatakayowasaidia uzeeni wakati aambao
hawatakuwa wakifanya tena sanaa.Alisema pia suala la haki miliki litakuwa miongoni mwa mada zitakazofundishwa kwenye semina hizo kwani suala hilo bado ni tatizo.
0 comments:
Post a Comment