Udaku matata Kabisa, Staa
wa Bongo Fleva, mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Estelina Sanga
‘Linah’ na mchumba’ke, Nangari Kombo wanadaiwa kutibuana, kisa kikidaiwa
ni maneno ya wanafiki yasiyokuwa na ukweli.
Habari za chini ya
kapeti zilinyetisha kwamba mtiti kati ya wawili hao ulijiri juzikati
baada ya Kombo kudaiwa kuanza kumtuhumu Linah kuwa anapokuwa kwenye
ziara za matamasha kama Fiesta huwa anamsaliti na wanaume wengine.
Chanzo hicho kilidai
kwamba, kufuatia madai hayo Kombo alimuanzishia Linah bonge la tafrani
na kujikuta kila mmoja anachukua hamsini zake.
Linah alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema: “Ni kweli kulitokea kutoelewana but (lakini) tumeyamaliza, tupo vizuri sana.”
Linah alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema: “Ni kweli kulitokea kutoelewana but (lakini) tumeyamaliza, tupo vizuri sana.”
0 comments:
Post a Comment