Michuano
ya Kombe la Kagame inaendelea kutimua vumbi leo kwa kuzikutanisha timu
ya APR SC kutoka Rwanda ikimenyana na LLB ya Burundi huku mchezo wa
kwanza ukizikutanisha Heegan FC ya Somalia na Al Shandy ya Sudan Uwanja
wa taifa jijini Dar es salaam.

Katika
matokeo ya jana uwanja wa taifa, mabingwa wa Tanzania bara, Young
Africans waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Telecom
kutoka nchini Djibout.
Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Malimi Busungu aliyefunga mabao mawili na Geofrey Mwashiuya aliyefunga bao la tatu kwa kombora kali umbali wa mita 20 na kupeleka kilio kwa timu ya Telecom.
Hata hivyo, Yanga walipoteza penati mbili zilizopigwa na washambuliaji wake Amisi Tambwe na Saimon Msuva zilizookolewa na mlinda mlango wa Telecom, Nzokira Jeef.
Katika mchezo wa uliotangulia mapema saa 8 mchana, timu Khartoum ilibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya KMKM, huku katika uwanja wa Karume KCCA ya Uganda ikiibuka na ushindi wa bao 1-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.

0 comments:
Post a Comment