Kumekuwa na mivutano kati ya wasanii wa Kimarekani kwenye mtandao wa Twitter, tumeyaona ya Meek Mill akimshabulia Drake na ya Nicki Minaj kushambulia tuzo za MTV VMA’s 2015.
Baada ya blogs na websites nyingi kumuunga mkono Nicki Minaj juu ya tuzo hizo, msanii Taylor Swift
ameaanza kuelewa sababu iliyomsukuma Nicki kuongea vile mtandaoni. Na
kuonyesha kuwa hana kinyongo msanii huyo alipost ujumbe twitter akisema…
>>>“nilihisi umenishambulia mimi kumbe haiko hivyo, nilikuelewa vibaya..samahani”. <<< Taylor Swift.
Nicki Minaj alianzisha mjadala kuhusu ubaguzi wa wasanii weusi wa kike kwenye Tuzo za MTV VMA’s Twitter huku akidai wasanii wakizungu hupendelewa zaidi, baada ya Taylor kusikia hivyo alimshambulia Nicki na kudai anashangazwa kwa nini yeye yupo mstari mbele kuwachonganisha wanawake kwenye industry.
Taylor Swift ana mtazamo wa tofauti kabisa sasa hivi juu ya malalamiko ya Nicki Minaj, Taylor alichukua time na kumuandikia Nicki Twitter kusema…
>>> “nilihisi
nashambuliwa mimi kama mimi, na hasira zilinifanya nisielewe point yako
na kunifanya kuongea vile… naomba unisamehe Nicki”. <<< Taylor Swift.
Nicki alijibu ujumbe huo kwa kusema kuwa yameisha na heshima yake juu ya Taylor imeongezeka na ni msanii wa kike mwenye mchango mkubwa kwenye muziki.
0 comments:
Post a Comment