Katika hali isiyo ya kawaida, amezaliwa mtoto wa kike asiyekuwa na ngozi ya huko India. Wataalamu katika hospitali aliyozaliwa binti huyo, wamesema kuwa amezaliwa na gongwa hatari la Genetic liitwalo Harlequin Ichthyosis.
Mtoto huyo aliezaliwa na binti wa miaka 23, Gonjwa hilo limepelekea ngozi yake kujigawanya katika sehemu chache mwilini na sehemu nyingine kubwa zimekuwa hazina ngozi kabisa.
Madaktari wa hospitali aliyozaliwa binti huyo, wamesema atahitaji matunzo ya muda mrefu sana hata maisha ili kuweza kupewa baadhi ya tiba zitakazopelekea kuundwa kwa ngozi mwilini kwa binti huyo, baadhi ya tiba hizo ni Petroleum Jelly na Mafuta ya nazi/ coconut oil.
Mtoto huyo aliezaliwa na kilo 1.8 ajabu lingine alilonalo ni kutokua na masikio lakini mfumo wa upumuaji wa mtoto huyo hauna shida kabisa.
Indian Press inadai kuwa kilichopelekea mtoto huyo kuzaliwa hivyo ni kukosa fedha kwa wazazi wake, swala lililopelekea kushindwa kuhudhuria kliniki wakat wa ujauzito.
Gonjwa hili halina tiba, na huwa ni nadra sana kutokea.. Mara ya mwisho lilimtokea mtoto mwaka 1994 huko USA na mtoto huyo aliishi hadi mwaka 2008.
SOURCE. India Press
Endelea kutembelea tedvibes.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment