Monday, June 13, 2016

Zito aonekana dar

Wakuu habarini.
tayari tupo makao makuu ya chama cha ACT WAZALENDO tunamsubili Kiongozi wa chama hicho Zitto Zuberi kabwe,
waandishi wamejitokeza wengi kweli kweli,
viongozi wa chama wanaendelea na maandalizi ya mkutano huo,
ndani ya dakika chache zijazo mkutano na waandishi unaanza.

live Updates zitawajia kupitia mimi mwenyewe.
karibuni

UPDATES
Tayari viongozi wanaelekea eneo la mkutano, waandishi nao wanaweka sawa vinasa sauti vyao na vinasa picha

nimedokezwa hapa zitto ataongelea masuala kadhaa

- namna Magufuli anavyominya Demokrasia
- kuzuiwa kwa Kongamano lao la jana pale Millenium Towers
- msimamo wao kama chama kuhusu hali inayoendelea
- way foward

nitaendelea kuwajuza

UPDATES
.......................
Zitto A mewasili
anasema hajui ni kwanini Polisi wamezuia Kongamano lao la Kuchambua Bajeti.

anasema
''juzi usiku siku ya jumaamosi, watu wetu wa usalama wa chama walinijulisha kwamba Jeshi la Polisi wananitafuta, wakaenda nyumbani kwangu na magari manne kunikamata bila kufuata utaratibu''

Zitto ''Jumanne iliyopita Kamishna Wambura alinipigia kuniomba nifike polisi''

Zitto ''Hii ya Jumaamosi walikuwa wanataka Kunivizia''

UPDATES
...................
Zitto ''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari'

Zitto '' Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa''

Zitto '' Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia''

UPDATES

Zitto ''Tunalaani tabia za KIDIKTETA za Rais Magufuli''

Zitto ''Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie''

UPDATES

Zitto ''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya RWANDA, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta''

Zitto '' Hauwezi kupamnana na UFISADI kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG''

UPDATES
...................
ZITTO ''Kwa hali Hii anayokwenda MAGUFULI AJIANDAE KUWA RAIS WA TERM MOJA kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa na Rais DIKTETA KAMA YEYE''

Zitto '' CCM wamdhibiti MAGUFULI, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti''

Zitto '' Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''

UPDATES
ZITTO ''IGP ameagizwa na MAGUFULI anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza klutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao''

UPDATES
ZITTO '' Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmeudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa''

UPDATES

Zitto '' Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

UPDATES

ZITTO ''CCM wamdhibiti mwanachama wao MAGUFULI, wasipomdhibiti sisi Tutamdhibiti''

MASWALI

Jambo leo
Naomba unikumbushe sheria inayoruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano na makongamano

ZITTO ''Sheria ya Vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 inaruhusu vyama vya siasa kufanya siasa, makongamano na mikutano ni sehemu ya siasa, hatuhitaji kuomba kibali

SWALI
Je mkutano utarushwa Live

Zitto ''Tutaweka Utaratibu ili watanzania wengi zaidi waweze kushiriki kwenya kongamano''

UPDATES
Zitto ''Polisi hawana mamlaka ya kisheria Kuzuia Mikutano ya vyama vya siasa, tunaipongeza Chadema kufungua kesi ya kikatiba mwanza, sisi tunafungua hapa Dar, na tunavitaka vyama vingine vifungue kesi ili ziwe nyingizaidi kudai haki''

UPDATES

Zitto ''Kama serikali haifanyi sawa sawa ni wajibu wetu kuwakosoa, na tutawakosoa tutawakosoa kama tulivyokuwa tukifanya serikali iliyopota...serikali ya sasa haina uvumilivu''

UPDATES
Zitto ''Bunge limenisimamisha Ubunge, tutatumia Forums nyingine kuwatetea wananchi na Demokrasia...Hatuhitaji kibali cha mtu yeyote kufanya kongamano''

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...