Sunday, July 3, 2016

Happy Birthday Esther machangu

Tarehe kama ya leo miaka kibao iliyopita alizaliwa huyu C.E.O wa Ted vibes anaitwa esther machangu mpambanaji mwanamke mwenye mipango kibao ya kuinua vipaji vya wasanii wa changa lakini pia kuwapa surport na kuwapamoyo wasichana wakitanzania kuwa wanaweza ni mwanaharakati wa kupigania wasichana kwanguvu.
Esther machangu ni mchanga wa marangu na anajihusisha na biashara lakini pia ni mtangazaji wa kituo cha radio cha fountain radio kilichopo mjini moshi.
Akiongea na tedvibes.com esther amesema kwenye siku yake hii ya leo atamweka kwanza mungu mbele kwa kumshukuru lakini pia kumwomba mungu ampe nguvu zaidi katika mapambano yake ya kiharakati kumkomboa mtoto wa kike lakini pia mtanzania kwa ujumla.
Moja ya vitu ambavyo esther alisha wahi kufanya ni pamoja na kuandaa event ya brighter ambayo ilikutanisha wanafunzi wa shule za sekondari mjini moshi lakini pia ameshafanya semina nyingi na wasichana wa shule za sekondari kwa nia ya kuwapa uwezo lakini pia kuwapa ujasiri wa kuwa wao pia wanaweza.
Ameongeza kuwa yeye kama yeye hii itakuwa siku yake kubwa na tofauti sana kwani anaiita it's me esther born again .
Kwenye kuweka sawa hili la born again ni kutokana nakuona mafanikio kila siku kwenye maisha yangu.kwa mujibu wa esther machangu.
Ted vibes inamtakia esther maisha mema na mungu aendelee kumlinda.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...