Monday, January 23, 2017

Juma Ali ndiye mbunge wa Dimani

ZANZIBAR: Mgombea Ubunge jimbo la Dimani kupitia tiketi ya CCM, Juma Ali Juma ameibuka mshindi baada ya kupata jumla ya kura 4860.

- Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Hafidh Ally Tahir kufariki dunia mwezi Novemba mwaka jana.

Treni yapata ajali

Takribani watu 36 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa baada ya Treni ya abiria kuacha reli kisha kupinduka.

- Inadaiwa kuwa idadi vya vifo huenda ikaongezeka kutokana na baadhi ya watu kujeruhiwa.

Friday, January 13, 2017

MOTO WAZUKA ARRIVAL HALL-JNIA


Moto mkubwa umezuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa leo na kusababisha taharuki kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, ambapo imelazimu shughuli zote uwanjani hapo kusitishwa kwa muda wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno ameuambia mtandao huu kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za kawaida zinaendelea kama kawaida.

Taarifa zaidi, zitatolewa baadaye.

*Source*GPL

Friday, October 7, 2016

Waziri mkuu wa umoja wa mataifa apatikana mpya

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa wingi wa kura limemteua aliyekuwa waziri mkuu wa Ureno Antonio Guterres kuwa katibu mkuu mpya wa umoja huo.

Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unatarajiwa kufanyika wiki ijayo kuidhinisha uchaguzi wake kwa muhula wa miaka mitano.

Bwana Guterres ,mwenye umri wa miaka 67,ambaye aliongoza kitengo cha wakimbizi katika Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka 10 atachukua mahala pake Ban Ki-moon mapema mwaka ujao.

Bwana Ban mwenye umri wa miaka 72,alimtaja bwana Guterres kama 'chaguo zuri' la kumrithi.

''Uzoefu wake kama waziri wa Ureno, ujuzi wake wa maswala tofauti duniani na ukakamavu wake utamsaidia katika kuliongoza shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika kipindi muhimu'' ,bwana Ban aliwaambia wanahabari alipozuru mjini Rome.

Wednesday, October 5, 2016

Raisi Magufuli apongezwa na serikali ya Ujerumani

Serikali ya Ujerumani imepongeza juhudi za Rais Dokta John Pombe Magufuli za kupambana kwa vitendo rushwa na ufisadi na kusema hatua hiyo inapaswa kuungwa mkono kwa dhati ambapo ujerumani imeahidi kuendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo huduma ya afya usambazaji maji vijijini pamoja na kuimarisha utawala bora.

Wajumbe 5 kati ya 9 wanaounda bodi ya Wadhamini CUF wakana uhalali wa maamuzi juu ya Prof. Lipumba

Bodi ya wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) imegawanyika baada ya wajumbe watano kati ya tisa wanaounda bodi hiyo kutoka Tanzania Bara kukana uhalali wa kikao kilichofanyika jana ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo .

Leo gazeti la kila Siku la Mwananchi limeripoti taarifa kuwa bodi ya wadhamini ya CUF imemkana Profesa Ibrahim Haruna Lipumba lakini taarifa za mchana huu ni kwamba wajumbe watano kati ya tisa wamepinga maamuzi ya kilichoitwa azimio la bodi ya wadhamini kumkana Lipumba

Monday, September 19, 2016

Mapambano ya idrissa yanaendelea

Mfanye @idrissultan a-host @MtvMamas 2016
Ni Rahisi gusa HAPA👇🏾halafu comment neno "YAY"

https://www.instagram.com/p/BKdf-Bqgfq7/

Au tembelea Page ya @mtvbaseafrica #Instagram #Facebook au #Twitter coment Neno YAY kwenye picha ya @idrissultan @mtvmamas #mtvmama2016
Neno ni YAY kwa herufi Kubwa kwenye Picha ya @idrissultan tu

#InfoPOWEREDBY: @kwanzapromo www.kwanzanetworks.com www.djhazuu.com @djhazuu @defxtro Cc. @carrymastory

Monday, August 15, 2016

Wizara ya maliasili na uchukuzi yatoa onyo kali

WIZARA ya Maliasili na Utalii imetoa onyo kwa yeyote  atakayejaribu  kudhoofisha  ama  kukwamisha  jitihada  za  kulinda  hifadhi  za  taifa ,mapori  ya  akiba  na  misitu huku ikitaka suala la mifugo kuingizwa katika hifadhi za taifa lisichukiliwe kisiasa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Mlele mkoani Katavi.

Alisema kwa watakao bainika kudhorotesha jitihada hizo watashughulikiwa  kikamilifu  kwa  mujibu   wa  sheria  na  kwamba   agizo   la  serikali   la  kuhakikisha  rasilimali  hizo   zinalindwa  kwa  faida  ya  kizazi  cha  sasa  na  kijacho  linatekelezwa  kwa  vitendo .

Milanzi alisistiza umuhimu  wa  kila mmoja  kutimiza  wajibu  wake  ukiwemo  wa  kuheshimu  sheria ili  kuepusha madhara  yasiyo  ya lazima  ambayo  licha  ya  kuchelewesha  maendeleo   yanawasababishia  wananchi   umaskini  usio  wa  lazima.

Kuhusu suala la mifugo ,Meja Jenerali Milanzi nguvu iongezwe katika kuitoa mifugo hiyo mara moja, ili kuzuia madhara makubwa yanayosababishwa na mifugo hiyo, ikiwa ni pamoja uharibifu mkubwa wa mazingira na kuenea kwa magonjwa ya mifugo.

Mkurugenzi  mkuu  wa  Tanapa  Bw  Allan  Kijazi  alisema  jitihada  za kuimarisha  ulinzi  zimeanza  kuzaa  matunda.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Fred  Manongi   alisema  mafunzo  ya jeshi  usu  ni  muhimu  kwa  watendaji  wote  wa  sekta  ya  uhifadhi.

Mwakilishi  kutoka  Shirika  la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi Getrude  Lyatuu amesema hatua  iliyofikiwa  inaanza  kurejesha  matumaini .

Saturday, August 6, 2016

Defao akwama mombasa hotelini

Mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo maarufu kama General Defao akwama hotelini jijini Mombasa baada ya kushindwa kulipa Bili ya Ksh 20,000.
Mkali huyo wa kutoka nchini kongowa miondoko ya rhumba amesema ameshindwa kulipa bills kutokana na kukosa kiasi cha sh. Ya kenya elfu 20000.
Ameongeza kuwa club iliyo mleta ndo wameshindwa kulipa bills za chakula na malazi na ukiangalia alikuwa amebokiwa tarehe 28 mwezi wa saba lakini meneja wa club hiyo akamwomba akae mpaka tarehe 3 ndo aweze perfom matokeo yake meneja aliye mweka akashindwa lipa bills za siku 4

Thursday, August 4, 2016

Tren lauwa dar

Treni inayotoka Stesheni ya Posta kwenda Pugu mida ya saa 12 jioni, iimesababisha mtu mmoja kufariki baada ya huyo mtu aliye dandia treni na kudondoka chini wakati likiwa katika mwendo. Kijana huyo ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja alidandia treni hiyo Wakati ikiwa Kamata Kariakoo kwenda Stesheni akiwa na lengo la kugeuza nalo kwenda Pugu.

Ndipo akalidandia likiwa kwenye mwendo huku milango ya treni ikiwa haijafunguliwa huku akiwa ananing’inia kwa nje ndipo alipojibamiza kwenye kingo za treni na kudondoka chini.

Story ya raisi wa simba ipo hapa


Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinadai kwamba, Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva anashilikiwa na Jeshi la polisi kwenye kituo cha Urafiki.

Aveva anashikiliwa na Polisi kwa bibali cha Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba na alipoulizwa ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo wa juu kabisa wa wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo wakiulizwa TAKUKURU.

“Kama unaweza labda ungewauliza watu wa TAKUKURU wanaweza wakajua ni lini uchunguzi wao utakamilika ni lini watampeleka mahakamani. Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi, vinginevyo wangekuwanae kule na wangejibu maswali yote ambayo wananchi wanataka kujua,” amesema Foibe kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni wakati anahojiwa na kituo kimoja cha radio cha jijini Dar es Salaam.

“Tunamshikilia, yupo kwenye mikono salama. Sisi tunaendelea na uchunguzi wetu, sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu,” amesema Musa Milaba afisa habari wa TAKUKURU.

Mchungaji afariki kutaka kuvunja rekodi ya yesu ya kufunga

Mchungaji wa Afrika Kusini Alfred Ndlovu (44) amefariki baada ya kufunga usiku na mchana kwa siku thelathini akitaka kuvunja rekodi ya Yesu Kristu aliyefunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa kitu chochote.

Mchungaji Alfred aliondoka nyumbani kwake tarehe 17/6/2016 na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka nia kwa Mungu na kujitenga na anasa za ulimwengu. Mchungaji huyu alijulikana kwa imani yake thabiti na familia yake pamoja na jamii iliyomzunguka waliamini imani yake ingeweza hata kuhamisha milima. Kifo chake kimeishangaza jamii nzima likiwemo Kanisa alilokuwa akihudumu.

Akijaribu kuvunja rekodi ya Yesu Kristu, Mchungaji Ndlovu alifariki baada ya kufunga kwa takribani mwezi mzima japokuwa hakuwahi kuripotiwa kuwa na ugonjwa wowote. Alikuwa peke yake nyikani na maiti yake ilionwa na mpita njia aliyetoa taarifa polisi

Wednesday, August 3, 2016

Bei ya mafuta yapanda tena

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kuanzia leo kutokana na mabadiliko ya bei katika Soko la Dunia.

Bei hizo za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote ya petroli, dizeli na taa zimepanda, ikilinganishwa na bei zilizotolewa mwezi uliopita.

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema bei za reja reja, zimeongezeka kwa Sh 17 kwa lita moja ya petroli sawa na asilimia 0.88, dizeli Sh 90 kwa lita sawa na asilimia 5.24 na mafuta ya taa Sh 72 kwa lita, sawa na asilimia 4.28 ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita.

Kwa upande wa bei za jumla, Mkurugenzi Mkuu huyo alisema pia zimeongezeka kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa, ambapo bei mpya za jumla zitakuwa Sh 16.56 kwa lita moja ya petroli sawa na asilimia 0.93, dizeli Sh 90.20 kwa lita sawa na asilimia 5.59 na mafuta ya taa Sh 72.29 kwa lita sawa na asilimia 4.58 .

Ngamlagosi alisema kuongezeka kwa bei hizo katika soko la ndani, kwa kiasi kikubwa kumetokana na kuongezeka kwa bei katika Soko la Dunia, na gharama za usafirishaji wa bidhaa hiyo kuja nchini.

Pamoja na mabadiliko hayo yanayoihusu nchi nzima, alisema bei hizo mpya, hazitauhusu mkoa wa Tanga ambapo vituo vya mafuta mkoani humo vimeagizwa kutopandisha bei mwezi huu.

Alisema hatua hiyo inatokana na mkoa huo, kutokupokea mafuta mapya mwezi Julai, na kufanya bei za Agosti kuendelea kutumika kama ilivyokuwa kwa mwezi Julai.

“Mamlaka (Ewura) inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika, zinapatikana vilevile kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo, ambapo huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkono nchini,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko.

Alisema Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta na kuongeza; “ Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.”

Alisema kampuni za mafuta, zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani, mradi tu bei hizo ziwe chini ya bei kikomo, kama ilivyokokotolewa na fomula iliyopitishwa na Ewura.

Alisema vituo vyote vya mafuta, vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango, yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kuhamasisha. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu huyo alisema adhabu kali, itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika. Alishauri wanunuzi kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo, inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Alisema stakabadhi hiyo ya malipo, itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta, endapo kutajitokeza malalamiko au kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo ; au atauziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

Tuesday, August 2, 2016

Mwalimu auwawa bariadi

Mwalimu Daniel Msalika (42) wa shule ya msingi Nyasosi, wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha.

Majeraha hayo yalitokana na kushambuliwa na baadhi ya wananchi kwa madai ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike wa shule hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga aliwaeleza waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa mwalimu huyo alifariki dunia Julai 31 mwaka huu saa nane usiku.

Kamanda Lyanga alisema kuwa siku ya tukio Julai 27 mwaka huu saa 6.30 usiku, wananchi hao ambao idadi yao haijafahamika, walivamia nyumba ya mwalimu huyo baada ya kupata taarifa kuwa kuna mwanafunzi ambaye amelala nyumbani kwake, jambo ambalo halikuwa la kweli.

“Wananchi hao walipata taarifa ya kuwa nyumbani kwa mwalimu kuna mwanafunzi ambaye amelala humo hivyo walimvamia kwa kuvunja mlango na kuanza kumshambulia kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi na kumsababishia majeraha makubwa sehemu za kichwani na usoni lakini binti waliyemkuta kwake ni mwenye umri wa miaka 18 na siyo mwanafunzi,” alisema.

Alisema kuwa baada ya uvamizi huo, mwalimu huyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Isanga kupatiwa matibabu, lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, lakini alifariki dunia.

Kamanda alisema kifo chake, kimesababishwa na majeraha ya kushambuliwa huku tuhuma dhidi yake zikiwa si za kweli.

Alitoa mwito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi huku wakisisitiza kuwa wote watakaobainika kusababisha kifo hicho, sheria itachukua mkondo wake.

IMF: Uchumi wa Tanzania waongoza Afrika Mashariki

Source BBC SWAHILI
Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.
Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.
Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .

Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.
IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.
Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.

Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.
Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.
Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.
Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
Ivory Coast 8.5%
Tanzania 6.9%
Senegal 6.6%
Kenya 6%
Zambia 3.4%
Nigeria 2.3%
Afrika Kusini 0.6%

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...