Monday, August 15, 2016

Wizara ya maliasili na uchukuzi yatoa onyo kali

WIZARA ya Maliasili na Utalii imetoa onyo kwa yeyote  atakayejaribu  kudhoofisha  ama  kukwamisha  jitihada  za  kulinda  hifadhi  za  taifa ,mapori  ya  akiba  na  misitu huku ikitaka suala la mifugo kuingizwa katika hifadhi za taifa lisichukiliwe kisiasa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Mlele mkoani Katavi.

Alisema kwa watakao bainika kudhorotesha jitihada hizo watashughulikiwa  kikamilifu  kwa  mujibu   wa  sheria  na  kwamba   agizo   la  serikali   la  kuhakikisha  rasilimali  hizo   zinalindwa  kwa  faida  ya  kizazi  cha  sasa  na  kijacho  linatekelezwa  kwa  vitendo .

Milanzi alisistiza umuhimu  wa  kila mmoja  kutimiza  wajibu  wake  ukiwemo  wa  kuheshimu  sheria ili  kuepusha madhara  yasiyo  ya lazima  ambayo  licha  ya  kuchelewesha  maendeleo   yanawasababishia  wananchi   umaskini  usio  wa  lazima.

Kuhusu suala la mifugo ,Meja Jenerali Milanzi nguvu iongezwe katika kuitoa mifugo hiyo mara moja, ili kuzuia madhara makubwa yanayosababishwa na mifugo hiyo, ikiwa ni pamoja uharibifu mkubwa wa mazingira na kuenea kwa magonjwa ya mifugo.

Mkurugenzi  mkuu  wa  Tanapa  Bw  Allan  Kijazi  alisema  jitihada  za kuimarisha  ulinzi  zimeanza  kuzaa  matunda.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Fred  Manongi   alisema  mafunzo  ya jeshi  usu  ni  muhimu  kwa  watendaji  wote  wa  sekta  ya  uhifadhi.

Mwakilishi  kutoka  Shirika  la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi Getrude  Lyatuu amesema hatua  iliyofikiwa  inaanza  kurejesha  matumaini .

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...