Wednesday, October 12, 2011

MWANAHIPHOP AMBAYE NI MEMBER WA kundi la GOOD MUSIC FAMILY lILIlOKO CHINI YA mkali KANYE WEST AMEFUNGUKIA MASHABIKI WAKE KUWA HATOIMBIA TENA CHINI YA KIVULI CHA LABLE YA hiyo ya G.O.O.D MUSIC.

KANYE WEST
COMMON ametangaza kuwa ujio wake mpya wa albamu yake mpya ya The Dreamer, The Believer, hatoiachia kupitia G.O.O.D. Music,Common anayetokea Chicago ameweka wazi kuwa hivi sasa haitaji tena msaada kutoka kwa kibopa wake  Kanye West ambaye ndiye aliyemsaidia mwaka 2005 wakati wa akiachilia albamu yake iliyoitwa ‘BE.’ 
                                        COMMON
Jamaa ameongeza kufunguka katika kituo Fulani cha tv kuwa yeye bado ni mmoja kati ya wana G.O.O.D. MUSIC FAMILY,ila hatofanya kazi chini ya label hiyo ikiwa ni albamu yake ya tisa ambayo itafanyika chini ya production za NO I.D. 

Common ameendelea kuwahakikishia fans wake juu ya habari za chinichini kuwa anatarajia kufanya collabo katika albamu moja na msaniiNAS kuwa ni kweli na wajiandae kwa hilo  japokuwa bado hawajaafiki jina la kutumia katika albamu hiyo ingawa kulipendekezwa jina la  Nas.com ambapo mwanzoni ndio lilikuwa kama title wakati 
                                     NAS NA COMMON
ilitegemewa kuwa ni Joint Mixtape kati ya  maveterani MCs hao. 

THE DREAMER, THE BELIEVER itaachiwa rasmi mnamo November 22 mwaka huu hapa. 

   

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...