Sunday, June 29, 2014

Noiz Mekah yatoa mixtape ya beat 10 za bure kwa msanii yeyote 'Biashara Ngumu'

Noiz Mekah yatoa mixtape ya beat 10 za bure kwa msanii yeyote
Studio za Noiz Makah chini ya Producer DX, zimetoa mixtape ya midundo ya hip hop 10 waliyoipa jina la Biashara Ngumu Volume 1, wanayoigawa bure kwa msanii yeyote wa Hip Hop.
DX aliiambia THADE EXPENSIVE  kuwa jina la mixtape hiyo, ‘Biashara Ngumu’ linatokana na aina ya midundo iliyomo ambapo midundo mitano ni ya Hip Hop biashara (laini) na mitano mingine ni Hip Hop ngumu.
Akieleza kuhusu lengo la kuitoa mixtape hiyo, DX amesema kuwa ni kusapoti wasanii hasa wachanga.
“Nia ya projet yenyewe ni kuweza kusapoti wasanii especially wasanii chipukizi kwa sababu kwenye tasnia ya muziki especially category ya Hip Hop tuna wasanii wengi chipukizi wanataka kuonesha ujuzi wao kupitia talent shows, kupitia hizi open stage/open mic na hat offer wanazopewa katika studio mbalimbali hapa Tanzania. Sasa sisi kama Noiz Mekah tumeona ni vizuri kusapoti.”
Ameeleza kuwa beat hizo zitaendelea kutoka kama mixtape na hiyo ni Volume 1, kwa hiyo zinakuja nyingine zaidi na zinapatikana bure kupitia website ya mkito.com.

No comments:

Post a Comment