Mashabiki wa soka nchini Uingereza wamegoma kuilaki timu yao wakati
ilipowasili jijini Manchester, ikitokea nchini Brazil ambapo ilikuwa
ikishiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.
Wakati kikosi cha Uingereza kikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa
Manchester, palionekana kimya, kama mashabiki wa soka walikuwa hawajui
kinachoendelea mara baada ya timu yao kushindwa kufurukuta kwenye
michezo ya kundi la nne ambalo liliijumuisha timu ya Italia, Uruguay
pamoja na Costa Rica.
Hata hivyo wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza walionekana
kutokuwa na furaha licha ya kurejea nyumbani salama, ambapo kila mmoja
alionekana anashuka kutoka kwenye ndege akiwa na begi pamoja na mfuko
mweupe ambao unahisiwa huenda ikiwa ni zawadi za familia zao.
Kitendo cha mashabiki wa Uingereza kuilaki timu yao huko Manchester
Airport, kimekuwa ni tofauti kubwa kilichoonekana katika nchi nyingine
zilizoshindwa kuendelea katika fainali za kombe la dunia, ambapo
imeonekana mashabiki wa nchi hizo kama Hispania wakijitokeza uwanja wa
ndege na kuonyesha upendo dhidi ya wachezaji wao.Uingereza iliondolewa kwenye fainali za kombe la duinia za mwaka huu
baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Italia mabao mawili kwa moja,
kisha ikafungwa idadi hiyo ya mabao dhidi ya Uruguay kabla ya
kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Costa Rica.
0 comments:
Post a Comment