Saturday, June 28, 2014

Uingereza warejea nyumbani , mashabiki wagoma kujitokeza uwanja wa ndege

Uingereza warejea nyumbani kama yatima, mashabiki wagoma kujitokeza uwanja wa ndege
Mashabiki wa soka nchini Uingereza wamegoma kuilaki timu yao wakati ilipowasili jijini Manchester, ikitokea nchini Brazil ambapo ilikuwa ikishiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.
Wakati kikosi cha Uingereza kikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Manchester, palionekana kimya, kama mashabiki wa soka walikuwa hawajui kinachoendelea mara baada ya timu yao kushindwa kufurukuta kwenye michezo ya kundi la nne ambalo liliijumuisha timu ya Italia, Uruguay pamoja na Costa Rica.
Hata hivyo wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza walionekana kutokuwa na furaha licha ya kurejea nyumbani salama, ambapo kila mmoja alionekana anashuka kutoka kwenye ndege akiwa na begi pamoja na mfuko mweupe ambao unahisiwa huenda ikiwa ni zawadi za familia zao.
Kitendo cha mashabiki wa Uingereza kuilaki timu yao huko Manchester Airport, kimekuwa ni tofauti kubwa kilichoonekana katika nchi nyingine zilizoshindwa kuendelea katika fainali za kombe la dunia, ambapo imeonekana mashabiki wa nchi hizo kama Hispania wakijitokeza uwanja wa ndege na kuonyesha upendo dhidi ya wachezaji wao.Uingereza iliondolewa kwenye fainali za kombe la duinia za mwaka huu baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Italia mabao mawili kwa moja, kisha ikafungwa idadi hiyo ya mabao dhidi ya Uruguay kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Costa Rica.

No comments:

Post a Comment