Tuesday, August 2, 2016

Kichanga chakanyagwa na gari

Mama mmoja ambaye bado hajajulikana eneo la Bunju B jijini Dar amekitelekeza pembezoni mwa barabara kichanga chake muda mchache baada ya kujifungua usiku wa kuamkia leo.

Amekitelekeza Pembezoni mwa barabara ya Bagamoyo Kihonzile na kwa bahati mbaya majira ya alfajiri kikakanyagwa na gari kabla ya kupata msamaria mwema.

Watu walioshuhudia tukio hilo na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wamesema, kitoto hicho kilikuwa kimefungwa kwenye mfuko wa plastiki hali iliyochangia gari ambalo halijajulikana kukikanyaga bila kujua kabla ya kupata wasamaria na wakiomba jeshi la polisi kushirikiana na wananchi kumsaka mzazi huyo kwa hatua zaidi za kisheria.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kihonzile Bw.Abdala Nzagi amesema alipewa taarifa majira ya alfajiri pamoja na kulaani kitendo cha kutekeleza kichanga hicho kwenye mfuko ameomba wananchi kutoa ushirikiano wa kumkamata mzazi huyo na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...