Tuesday, August 2, 2016

PLATNUMZ NA NDOTO ZA KUKUTANA NA BAHRKRESAA

Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Diamond platnumz amesema kuwa kati ya mtu anaetamani kukutana nae hapa Tz 255 ni Mmiliki wa kampuni ya Azam, Said Salim Bahkresa.
Platnum amesema hayo kaika kipindi cha leo tena cha Clouds Fm, pale alipoulizwa kwamba "anatamani sana kukutana na nani Tz" , platnumz alijibu kuwa  anatamani sana kukutana na Bahkresa
Aidha platnumz amesema kuwa anatamani sana kukutana mfanyabiashara huyo ili amuulize kuhusiana na kufanikiwa ku'manage biashara zake ilihali ni nyingi na kubwa sana.
Vilevile, platnumz ameweka wazi kuwa nia yake ni kuwa mfanyabiashara mkubwa na mziki anautumia kama njia ya kumfanikisha kufikia malengo yake.
Aidha Platnumz ameongeza kuwa jina Chibu Dangote amelichagua likiendana na tafsiri Big Boss.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...