Tuesday, November 8, 2011

DOCTOR WA MICHAEL JACKSON KIZIMBANI TENA

 Daktari wa Michael Jakson, Dk Conrad Murray amekutwa na kosa la mauaji bila kukusudia na mahakama moja mjini Los Angeles, Marekani.
 wazee wa mahakama ya Los Angeles - wanaume saba na wanawake watano Baraza la wazee hao lililoundwa na wazungu weupe sita, Mmarekani mweusi mmoja na Wamarekani watano wenye asili ya Hispania - walijadili shauri hilo kuanzia Ijumaa hadi Jumatatu asubuhi.
walichukua siku mbili kujadili kesi na kufikia hukumu hiyo.
Murray, 58, anaweza kukabiliwa na adhabu kamili ya kwenda gerezani kwa miaka minne na kupoteza leseni yake ya uganga.
Wanasheria wa Dk Murray walihoji kuwa Michael Jackson alijidunga mwenyewe dawa hiyo wakati daktari wake akiwa nje ya chumba.
Dk Murray alipelekwa rumande baada ya kukutwa na hatia na atasalia huko hadi wakati atakaposomewa adhabu yake, inayotarajiwa kutolewa Novemba 29.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...