Amesema jijini Dar es salaam viwanda viko vingi, na
vinahitaji umeme wa bei nafuu, kwakua sasa hivi zinatumika fedha nyingi
sana kwa ajili ya kununua afuta ya
disel, pamoja na mafuta mazito kwa ajili ya kuendesha mitambo, ambapo hugharimu
kiasi cha shilingi trilioni 1.6 kwa ajili ya gharama za mafuta peke yake.
Mh. Pinda amemaliza kwa kusema kua vurugu, na uvunjifu wa
amani hazita saidia bali kuharibu, na kuwapa pole wote wote walio ondokewa na
ndugu zao katika vurugu hizo, pamoja na viongozi na wananchi walio haribiwa
mali zao, na serekali itarudisha mapema huduma zilizo athiriwa na vurugu hizo.
Ameongeza kua wana Mtwara wanapaswa kutambua kua sababu ya
serekali kuomba sehemu ya gesi hiyo, iende ikasaidie jijini la Dar es salaam ni
upungufu mkubwa walio nao kama Taifa.
Vurugu zilizojitokeza hivi karibuni mkoani Mtwara,
zimetokana na kutokuwepo kwa maelezo sahihi.
Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na Waziri mkuu Mh.
Mizengo Kayanza Peter Pinda kabla ya kuanza kipindi cha masawali na majibu,
kama ilivyotaratibu za siku ya alhamisi katika kipindi cha bunge.
Mh. Pinda amesema kua kwa upande mwingine jambo hilo,
lilikua na upotoshaji mkubwa ambapo mwingine ulikua wa kiuchochezi, na wengine kufanya bila kujua.
Aidha amesema kua kuna taarifa ambazo zilichangia sana
kukuza tatizo, kua gesi iliyogundulika inahamishwa kupelekwa Bagamoyo
wakihusisha na uwepo wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete kuwepo Bagamoyo, jambo ambalo amesisitiza si kweli.
0 comments:
Post a Comment