Thursday, February 7, 2013

Kama ulimis story za show ya full p na EXPENSIVE



Za kijamii
RAIS Jakaya Kikwete amesema utawala wa sheria unatakiwa kulindwa kama mboni ya jicho na kuhakikisha haki na usawa vinatolewa bila ubaguzi.
 Alisema mahakama ni lazima iwe mahali pa kupata haki bila dhuluma wala kuonewa ili hisia za jamii kwamba haki inanunuliwa ziondoke, kwani zinatia doa hasa ikizingatiwa kuwa rushwa na utawala wa sheria haviendi pamoja.
 Akizungumza jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini na maadhimisho ya kuashiria mwanzo wa vikao vya mahakama, Kikwete alisema kuwa dhana ya mgawanyo wa mahakama unabidi ihesimiwe na kutambulika bila kuingiliwa katika utendaji kazi zake.
 Alitaka nakala za hukumu kutolewa kwa wakati na kusisitiza mawakili, wapelelezi na mahakimu kwa ujumla wasikilize mashauri kwa wakati ili kupunguza malalamiko.
 Naye Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, alisema kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba ni lazima mahakama ihakikishe inatenda haki.
 Alisema kuwa ni lazima kuwepo na udhibiti wa madaraka ya utawala wa kidikteta na ubinafsi.
 Pia Chande alitoa wito kwa Bunge kuangalia sheria ya makosa ya jinai na kumuadabisha mtu ambaye hakuweza kutoa msaada kwa aliye hatarini kudhurika ama kutolewa uhai.
 Aliongeza kuwa, kwa sasa wameanza uhakiki wa mashauri yote ili kusiwe na kesi itakayozidi miaka miwili kabla haijamalizika.
 Chande pia alikemea tabia ya kujichukulia sheria mkononi kunakofanywa na wananchi na kusema kuwa ni udhaifu wa utawala wa sheria unaosababishwa na ukosefu wa imani na vyombo vya dola, hasa Jeshi la Polisi, kukatishwa tamaa na mfumo mzima wa utoaji haki na kasi ya ahakama ya kumaliza mashauri.
===========.
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA) ameibana serikali na kuitaka ieleze kwanini imeutelekeza uwanja wa ndege wa Moshi.
 Alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza na kuihoji serikali ni kwanini imeutelekeza uwanja wa ndege wa Moshi wakati ni wa muhimu kwa wananchi wa wilaya hiyo.
 Awali katika swali la msingi mbunge huyo aliitaka serikali ieleze kama ni sahihi kuutelekeza uwanja huo ambao ni mlango wa kupanda Mlima Kilimanjaro.
 Pia alitaka serikali ieleze ni sababu zipi zimeifanya itelekeze uwanja huo ambao ni hazina kwa nchi.
 Katika swali hilo lililokuwa na sehemu tatu, alitaka serikali ieleze kama ilishawahi kutoa taarifa iwapo fedha za matengenezo ya uwanja huo zimeishatengwa hadi kufikia sasa, na kama kuna kilichofanyika ama serikali inasema uongo.
 Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, alisema  serikali haina lengo la kukiua na kukitelekeza kiwanja hicho kwa kuwa kina umuhimu kwa nchi.
 Alisema kuwa kiwanja hicho kina umuhimu wa kuwasafirisha na kuwahudumia watalii wanaokwenda Mlima Kilimanjaro na mbuga ya wanyama ya Kilimanjaro (KINAPA).
 Tizeba alisema umuhimu wa kiwanja hicho ni pamoja na kubeba wagonjwa wanaotaka kupata matibabu ya haraka kutoka katika hospitali ya rufaa ya KCMC au katika hospitali zingine ndani na nje ya nchi.
 Naibu Waziri alisema kiwanja hicho bado kinahudumiwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na hadi sasa kina wafanyakazi sita.
 “Kiwanja cha Ndege cha Moshi ni moja kati ya viwanja 10 vya ndege ambavyo Serikali imepanga kuviboresha kupitia mkopo kutoka Benki ya Dunia na katika awamu hii jumla ya sh bilioni 3.2 tayari zimepatikana kwa ajili ya kufanya upembuzi katika viwanja hivyo,” alisema Naibu Waziri.
==========.
Burudani
MSANII nyota wa filamu nchini, Mahfudh Hussein ‘Dk. Cheni’ amebainisha kuwa, hivi sasa wako katika maandalizi ya kucheza filamu na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’, aliyetoka mahabusu hivi karibuni.
 Lulu alikuwa mahabusu tangu Aprili 7 mwaka jana, akikabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia, aliyekuwa msanii nguli, Steven Kanumba.
 Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu juzi, Cheni alisema mpango huo umekuja baada ya Lulu kuwa nje ya ulingo wa filamu kwa zaidi ya miezi saba kutokana na kesi yake inayomkabili.
 Alisema hivi sasa Lulu ana kiu ya kucheza filamu, ikiwa ni katika kudhihirisha kipaji chake, hivyo wamepanga atacheza na kulipwa kiwango cha juu cha fedha kama mchezaji nyota na siyo mchezaji aliyeshirikishwa.
 “Tutamlipa fedha nyingi Lulu, kwa sababu yeye ni msanii nyota mwenye mvuto, huku jamii ikiwa na kiu ya kuona kazi zake ambazo hajazifanya kwa muda sasa,” alisema Cheni.
 Alisema kuwa, katika filamu hiyo pia atakuwepo msanii Steve Mengele ‘Steve Nyerere’, ambaye kwa pamoja ndio waliojitokeza kumpa sapoti Lulu.
 Katika hatua nyingine, Dk. Cheni ambaye yuko karibu zaidi na familia ya akina Lulu, alitanabaisha kuwa, tayari wameshampata mshauri nasaha kwa kumshauri Lulu ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya matatizo yaliyotokea.
===========.
   

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Dorice Mkangama, yuko mbioni kukamilisha kurekodi albamu zake mbili na kuziingiza sokoni hivi karibuni.
 Akizungumza na Tanzania Daima, Mkangama alizitaja albamu hizo kuwa ni ‘Namngoja Yesu’ ambayo ni ya nne na ‘Mvua ya Baraka’ ikiwa ni ya tano tangu alipoanza kuingiza sokoni albamu zake katika uimbaji wa nyimbo za injili.
 Alisema kuwa, kwa sasa matarajio yake makubwa ni kuingiza sokoni albamu mbili kwa mpigo, baada ya kukaa kimya muda mrefu.
 “Nilianza kuimba nyimbo za muziki wa injili tangu mwaka 2005 nikianza na albamu ya ‘Tazama Bwana’ kisha ya pili iitwayo ‘Yesu Namba Moja’ ambayo baadaye ilifuatiwa na ‘Mikononi mwa Yesu’.
 “Na sasa ninakuja na albamu hizo mbili, ambazo naamini wapenzi wa muziki wa Injili wakizipata watazifurahia, kwani nimeimba hasa na nimeongeza ubunifu wa hali ya juu,” alisema Dorice.
 Alisema ingawa jina lake halijawa kubwa kwenye muziki huo kama walivyo baadhi ya waimbaji wengine, ana uhakika ipo siku atafikia hali hiyo na kwamba, Mungu haruhusu watu wake kukata tamaa.
 “Ndiyo maana ninaendelea kuandaa albamu zaidi, nikiamini kwamba ipo siku jina langu litakuwa kubwa katika kazi hii ya kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji,” alisema.
=======================.
 Big brother na TID
Baada ya jana kusikia kuwa q chifu kachukua form TID nayeye naye kachukua form ya kushiriki big brother  na kufiksha idadi ya wasanii wa ongo kuwekahistoria ya kuchukua form za big brother ambako wema sepetu na nyeye aliichukua q cheaf na hemed pia wato kwenye nia ya kubeba kitita cha dola za kimarekani 300,000
Mshiriki wa mwaka jana Julio aliongea nakusema mtu kama TID angefaa sana kushiriki shindano hilo maana ni mcheshi na ana vigezo vingi vitavyomuwezesha kushinda.
================.
Kutoka kwa motto wa pwani chibow
Katiika halii ya kufanya yakamiliike kwenye game ya mzikii kwa mwezi huu wa piili chibow ametangaza kukamilisha rasmi kazi yake aliyo sema kuwa ni zawadi ya valentine kwa mashabiki wake na siku ya jumatatu ataiweka hewani watu waipate rasmi hajaweka wazi jna la wimbo wala prodaction na kudai na surprise tu kwa mafuns stay tune.
=================.
Dyana tena na blue
Dyana ni mmoja kati ya wadada walio juu kwasasa kwenye game ya mzikii ambako alitamba na ngoma kali kama vile Mafungu Ya Nyanya, Nivute Kwako na kumweka pazuri zaidi sasa ivi anakuja na kzi aliyo fanya na mr blue na ameamua kuachia cover arts ya ngoma hiyo hii leo jna la ngoma hiyo amesema inaitwa ''LEO''.
========.
 
Kazi imeanza kwa flaviana
Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania, Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESEL na EDUN. Kampeni hiyo inayoitwa DIESEL + EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya DIESEL - Renzo Rosso - na waanzalishi wa kampuni ya EDUN - Ali Hewson na Bono walisafiri nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Africa.
Waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.
Mwanamitindo Flaviana Matata ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni za nguo hizo.

 Habari za biashara
Alicho sema pinda
Waziri mkuu mizengo panda amewataka watanzania wasiwe na matumain ya muda mfupi au mategemeo pa ya muda mfupi kuhusu upatikanaj wa wa nishart ya petrol na gesi nchini.
Akifungua mkutano wa sita wa wadau wa nishati hiyo wan chi za afrika mashariki mjinii arusha jana alisema nishati hiyo inahitaji uwekezaji mkubwa hadi ianze kutoa matunda.
Aliwataka watanzaniia wawe tayari kujipanga vizuri katika kuimarisha kwa ushirikano kati ya wawekezaji na serikaliambayo jukumu lake nikujenga mazingira mazuri kwa wawekezaji.
Alisema kukuwakwa sekta y ages nay a petrol katika nchi za eac kutachochea ukuaji wa wa maendeleo katika nmaeneo mengne yakiwemo ya uchumi na ustawi wa jamii waziiri mkuu amesema kuwa ufahamu mdogo mongoni mwa wanachi hasa watanzania ni chnagamoto kubwa kwenye secta hiii.
Aliongeza kuwa jambo la msingi ni kuimarisha ushiriikiano katika nchi zote bza afrika masharikikatika utafiti wa uchimbajii na uzalishaji wa nishati zote kama hakuta kuwa na ushirikiano katka nchi zote ili kupata maendeleo.
===========.

 Mjue Shabani Robert
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari, 1909 kijiji cha Vibambani jirani na Machui kilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga, alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-salaam kati ya miaka 1922 na 1926 alifaulu na kupata cheti.
Akaajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani mwaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu kumesaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.
Tangu 1944 alihamia ofisi nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mbali na maandio yake alikuwa na athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa kamati za East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na Tanganyika Languages Board.
Kwa ujumla Mzee Shaaban Robert aliandika vitabu ishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni: Adili na Nduguze, Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad, Baada ya Miaka Hamsini, na Maisha Yangu. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha za Kichina, Kiingereza na Kirusi. Alifariki dunia tarere 22 Juni, 1962 na kuzikwa Machui. Aliacha wake watatu na watoto kumi.
Wazazi wake wote wawili walikuwa wa ukoo wa Mganga wa kabila la Kiyao. Hatujui sana habari za wazazi wake, lakini twajua kwamba jina la baba yake halikuwa Robert. Jina hili ama latokana na matamshi mabaya ya jina lake hasa au yawezekana kuwa ni jina alilopewa alipokuwa skuli Msimbazi. Kwa muda mfupi yeye mwenyewe aliandika jina lake ‘Roberts’, lakini baadaye aliacha kuliandika hivyo. Alizaliwa Vibambani, ambacho ni kijiji kilicho kusini ya Machui, yapata maili sita kusini ya Tanga, tarehe mosi January mwaka wa 1909. Hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita Waswahili.
Kazi alizofanya alipokuwa Karani wa Serikali:
Forodhani Pangani na mahali pengine tokea mwaka 1926 mpaka 1944
Idara ya Wanyama tokea mwaka 1944 hata 1946
Afisi ya Mkuu wa Jimbo Tanga tokea mwaka 1946 hata 1952
Afisi ya Kupima Nchi Tanga tokea mwaka 1952 hata 1960.
Alipandishwa cheo kuwa Grade III Higher Division mwaka 1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena kuwa Grade II Local Service Alikuwa mwanachama wa East African Swahili Committee, East African Literature Bureau, Tanganyika Languages, Tanga Township Authority
Alielemishwa Dar es Salaam toka mwaka wa 1922 mpaka mwaka wa 1926, akawa mtu wa pili katika wanafunzi kumi na mmoja waliofaulu mitihani yao na kupewa shahada ya kutoka chuoni, yaani School Leaving Certificate. Alioa mara tatu: mke wa kwanza alikuwa Mdigo. Alikuwa na watoto kumi. Alipofariki aliacha watoto watano. Pia aliacha dada yake (wa baba mmoja) Mwana Saumu, na Mama Yake.
Marehemu akafariki Tanga tarehe ya 22 Juni, 1962, akazikwa Machui.
Alitunza kwa zawadi ya waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa nishani ya M.B.E.
Vitabu vyake
Maisha yangu
Kusadikika nchi iliyo angani
Kufikirika
Adili na nduguze
Masomo yenye adili
Utenzi wa Vita vya Uhuru
Wasifu wa Siti Binti Saad
Baada ya Miaka Hamsini
=======

2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...