Za
kijamii
RAIS Jakaya Kikwete amesema
utawala wa sheria unatakiwa kulindwa kama mboni ya jicho na kuhakikisha haki na
usawa vinatolewa bila ubaguzi.
Alisema mahakama ni lazima iwe mahali pa
kupata haki bila dhuluma wala kuonewa ili hisia za jamii kwamba haki
inanunuliwa ziondoke, kwani zinatia doa hasa ikizingatiwa kuwa rushwa na
utawala wa sheria haviendi pamoja.
Akizungumza jana wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Sheria nchini na maadhimisho ya kuashiria mwanzo wa vikao vya mahakama,
Kikwete alisema kuwa dhana ya mgawanyo wa mahakama unabidi ihesimiwe na
kutambulika bila kuingiliwa katika utendaji kazi zake.
Alitaka nakala za hukumu kutolewa kwa wakati
na kusisitiza mawakili, wapelelezi na mahakimu kwa ujumla wasikilize mashauri
kwa wakati ili kupunguza malalamiko.
Naye Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, alisema
kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba ni lazima mahakama ihakikishe
inatenda haki.
Alisema kuwa ni lazima kuwepo na udhibiti wa
madaraka ya utawala wa kidikteta na ubinafsi.
Pia Chande alitoa wito kwa Bunge kuangalia
sheria ya makosa ya jinai na kumuadabisha mtu ambaye hakuweza kutoa msaada kwa
aliye hatarini kudhurika ama kutolewa uhai.
Aliongeza kuwa, kwa sasa wameanza uhakiki wa
mashauri yote ili kusiwe na kesi itakayozidi miaka miwili kabla haijamalizika.
Chande pia alikemea tabia ya kujichukulia
sheria mkononi kunakofanywa na wananchi na kusema kuwa ni udhaifu wa utawala wa
sheria unaosababishwa na ukosefu wa imani na vyombo vya dola, hasa Jeshi la
Polisi, kukatishwa tamaa na mfumo mzima wa utoaji haki na kasi ya ahakama ya
kumaliza mashauri.
===========.
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon
Ndesamburo (CHADEMA) ameibana serikali na kuitaka ieleze kwanini imeutelekeza
uwanja wa ndege wa Moshi.
Alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati
alipokuwa akiuliza swali la nyongeza na kuihoji serikali ni kwanini
imeutelekeza uwanja wa ndege wa Moshi wakati ni wa muhimu kwa wananchi wa
wilaya hiyo.
Awali katika swali la msingi mbunge huyo
aliitaka serikali ieleze kama ni sahihi kuutelekeza uwanja huo ambao ni mlango
wa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Pia alitaka serikali ieleze ni sababu zipi
zimeifanya itelekeze uwanja huo ambao ni hazina kwa nchi.
Katika swali hilo lililokuwa na sehemu tatu,
alitaka serikali ieleze kama ilishawahi kutoa taarifa iwapo fedha za
matengenezo ya uwanja huo zimeishatengwa hadi kufikia sasa, na kama kuna
kilichofanyika ama serikali inasema uongo.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi,
Charles Tizeba, alisema serikali haina
lengo la kukiua na kukitelekeza kiwanja hicho kwa kuwa kina umuhimu kwa nchi.
Alisema kuwa kiwanja hicho kina umuhimu wa
kuwasafirisha na kuwahudumia watalii wanaokwenda Mlima Kilimanjaro na mbuga ya
wanyama ya Kilimanjaro (KINAPA).
Tizeba alisema umuhimu wa kiwanja hicho ni
pamoja na kubeba wagonjwa wanaotaka kupata matibabu ya haraka kutoka katika
hospitali ya rufaa ya KCMC au katika hospitali zingine ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri alisema kiwanja hicho bado kinahudumiwa
na Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na hadi sasa
kina wafanyakazi sita.
“Kiwanja cha Ndege cha Moshi ni moja kati ya
viwanja 10 vya ndege ambavyo Serikali imepanga kuviboresha kupitia mkopo kutoka
Benki ya Dunia na katika awamu hii jumla ya sh bilioni 3.2 tayari zimepatikana
kwa ajili ya kufanya upembuzi katika viwanja hivyo,” alisema Naibu Waziri.
==========.
Burudani
MSANII nyota wa filamu nchini,
Mahfudh Hussein ‘Dk. Cheni’ amebainisha kuwa, hivi sasa wako katika maandalizi
ya kucheza filamu na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’, aliyetoka mahabusu hivi
karibuni.
Lulu alikuwa mahabusu tangu Aprili 7 mwaka
jana, akikabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia, aliyekuwa msanii nguli,
Steven Kanumba.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu
juzi, Cheni alisema mpango huo umekuja baada ya Lulu kuwa nje ya ulingo wa
filamu kwa zaidi ya miezi saba kutokana na kesi yake inayomkabili.
Alisema hivi sasa Lulu ana kiu ya kucheza
filamu, ikiwa ni katika kudhihirisha kipaji chake, hivyo wamepanga atacheza na
kulipwa kiwango cha juu cha fedha kama mchezaji nyota na siyo mchezaji
aliyeshirikishwa.
“Tutamlipa fedha nyingi Lulu, kwa sababu yeye
ni msanii nyota mwenye mvuto, huku jamii ikiwa na kiu ya kuona kazi zake ambazo
hajazifanya kwa muda sasa,” alisema Cheni.
Alisema kuwa, katika filamu hiyo pia atakuwepo
msanii Steve Mengele ‘Steve Nyerere’, ambaye kwa pamoja ndio waliojitokeza
kumpa sapoti Lulu.
Katika hatua nyingine, Dk. Cheni ambaye yuko
karibu zaidi na familia ya akina Lulu, alitanabaisha kuwa, tayari wameshampata
mshauri nasaha kwa kumshauri Lulu ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida
baada ya matatizo yaliyotokea.
===========.
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili,
Dorice Mkangama, yuko mbioni kukamilisha kurekodi albamu zake mbili na
kuziingiza sokoni hivi karibuni.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mkangama
alizitaja albamu hizo kuwa ni ‘Namngoja Yesu’ ambayo ni ya nne na ‘Mvua ya
Baraka’ ikiwa ni ya tano tangu alipoanza kuingiza sokoni albamu zake katika
uimbaji wa nyimbo za injili.
Alisema kuwa, kwa sasa matarajio yake makubwa
ni kuingiza sokoni albamu mbili kwa mpigo, baada ya kukaa kimya muda mrefu.
“Nilianza kuimba nyimbo za muziki wa injili
tangu mwaka 2005 nikianza na albamu ya ‘Tazama Bwana’ kisha ya pili iitwayo
‘Yesu Namba Moja’ ambayo baadaye ilifuatiwa na ‘Mikononi mwa Yesu’.
“Na sasa ninakuja na albamu hizo mbili, ambazo
naamini wapenzi wa muziki wa Injili wakizipata watazifurahia, kwani nimeimba
hasa na nimeongeza ubunifu wa hali ya juu,” alisema Dorice.
Alisema ingawa jina lake halijawa kubwa kwenye
muziki huo kama walivyo baadhi ya waimbaji wengine, ana uhakika ipo siku
atafikia hali hiyo na kwamba, Mungu haruhusu watu wake kukata tamaa.
“Ndiyo maana ninaendelea kuandaa albamu zaidi,
nikiamini kwamba ipo siku jina langu litakuwa kubwa katika kazi hii ya
kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji,” alisema.
=======================.
Big
brother na TID
Baada ya jana kusikia kuwa q
chifu kachukua form TID nayeye naye kachukua form ya kushiriki big brother na kufiksha idadi ya wasanii wa ongo
kuwekahistoria ya kuchukua form za big brother ambako wema sepetu na nyeye aliichukua
q cheaf na hemed pia wato kwenye nia ya kubeba kitita cha dola za kimarekani
300,000
Mshiriki wa mwaka jana Julio
aliongea nakusema mtu kama TID angefaa sana kushiriki shindano hilo maana ni
mcheshi na ana vigezo vingi vitavyomuwezesha kushinda.
================.
Kutoka
kwa motto wa pwani chibow
Katiika halii ya kufanya
yakamiliike kwenye game ya mzikii kwa mwezi huu wa piili chibow ametangaza
kukamilisha rasmi kazi yake aliyo sema kuwa ni zawadi ya valentine kwa
mashabiki wake na siku ya jumatatu ataiweka hewani watu waipate rasmi hajaweka
wazi jna la wimbo wala prodaction na kudai na surprise tu kwa mafuns stay tune.
=================.
Dyana
tena na blue
Dyana ni mmoja kati ya wadada
walio juu kwasasa kwenye game ya mzikii ambako alitamba na ngoma kali kama vile
Mafungu Ya Nyanya, Nivute Kwako na kumweka pazuri zaidi sasa ivi anakuja na kzi
aliyo fanya na mr blue na ameamua kuachia cover arts ya ngoma hiyo hii leo jna
la ngoma hiyo amesema inaitwa ''LEO''.
========.
Kazi
imeanza kwa flaviana
Mwanamitindo wa kimataifa
kutoka nchini Tanzania, Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo
makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESEL na EDUN. Kampeni hiyo inayoitwa DIESEL +
EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya
DIESEL - Renzo Rosso - na waanzalishi wa kampuni ya EDUN - Ali Hewson na Bono
walisafiri nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani
Africa.
Waliingia makubaliano ya
kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na
hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama
kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo zitaanza kupatikana
mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na duniani.
Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.
Mwanamitindo Flaviana Matata
ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee
kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni za nguo hizo.
Habari
za biashara
Alicho
sema pinda
Waziri mkuu mizengo panda
amewataka watanzania wasiwe na matumain ya muda mfupi au mategemeo pa ya muda
mfupi kuhusu upatikanaj wa wa nishart ya petrol na gesi nchini.
Akifungua mkutano wa sita wa
wadau wa nishati hiyo wan chi za afrika mashariki mjinii arusha jana alisema
nishati hiyo inahitaji uwekezaji mkubwa hadi ianze kutoa matunda.
Aliwataka watanzaniia wawe
tayari kujipanga vizuri katika kuimarisha kwa ushirikano kati ya wawekezaji na
serikaliambayo jukumu lake nikujenga mazingira mazuri kwa wawekezaji.
Alisema kukuwakwa sekta y ages
nay a petrol katika nchi za eac kutachochea ukuaji wa wa maendeleo katika
nmaeneo mengne yakiwemo ya uchumi na ustawi wa jamii waziiri mkuu amesema kuwa
ufahamu mdogo mongoni mwa wanachi hasa watanzania ni chnagamoto kubwa kwenye
secta hiii.
Aliongeza kuwa jambo la msingi
ni kuimarisha ushiriikiano katika nchi zote bza afrika masharikikatika utafiti
wa uchimbajii na uzalishaji wa nishati zote kama hakuta kuwa na ushirikiano
katka nchi zote ili kupata maendeleo.
===========.
Mjue
Shabani Robert
Shaaban Robert alizaliwa tarehe
1 Januari, 1909 kijiji cha Vibambani jirani na Machui kilomita 10 kusini mwa
mji wa Tanga, alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-salaam
kati ya miaka 1922 na 1926 alifaulu na kupata cheti.
Akaajiriwa na serikali ya
kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani mwaka 1926 – 1944.
Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa
mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu kumesaidia maendeleo yake
Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.
Tangu 1944 alihamia ofisi
nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mbali na maandio yake alikuwa
na athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa kamati
za East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na Tanganyika
Languages Board.
Kwa ujumla Mzee Shaaban Robert
aliandika vitabu ishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni: Adili na Nduguze,
Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad, Baada ya Miaka Hamsini, na
Maisha Yangu. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha za Kichina, Kiingereza na
Kirusi. Alifariki dunia tarere 22 Juni, 1962 na kuzikwa Machui. Aliacha wake
watatu na watoto kumi.
Wazazi wake wote wawili
walikuwa wa ukoo wa Mganga wa kabila la Kiyao. Hatujui sana habari za wazazi
wake, lakini twajua kwamba jina la baba yake halikuwa Robert. Jina hili ama
latokana na matamshi mabaya ya jina lake hasa au yawezekana kuwa ni jina
alilopewa alipokuwa skuli Msimbazi. Kwa muda mfupi yeye mwenyewe aliandika jina
lake ‘Roberts’, lakini baadaye aliacha kuliandika hivyo. Alizaliwa Vibambani,
ambacho ni kijiji kilicho kusini ya Machui, yapata maili sita kusini ya Tanga,
tarehe mosi January mwaka wa 1909. Hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa
mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita Waswahili.
Kazi alizofanya alipokuwa
Karani wa Serikali:
Forodhani Pangani na mahali
pengine tokea mwaka 1926 mpaka 1944
Idara ya Wanyama tokea mwaka
1944 hata 1946
Afisi ya Mkuu wa Jimbo Tanga
tokea mwaka 1946 hata 1952
Afisi ya Kupima Nchi Tanga
tokea mwaka 1952 hata 1960.
Alipandishwa cheo kuwa Grade
III Higher Division mwaka 1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena kuwa
Grade II Local Service Alikuwa mwanachama wa East African Swahili Committee,
East African Literature Bureau, Tanganyika Languages, Tanga Township Authority
Alielemishwa Dar es Salaam toka
mwaka wa 1922 mpaka mwaka wa 1926, akawa mtu wa pili katika wanafunzi kumi na
mmoja waliofaulu mitihani yao na kupewa shahada ya kutoka chuoni, yaani School
Leaving Certificate. Alioa mara tatu: mke wa kwanza alikuwa Mdigo. Alikuwa na
watoto kumi. Alipofariki aliacha watoto watano. Pia aliacha dada yake (wa baba
mmoja) Mwana Saumu, na Mama Yake.
Marehemu akafariki Tanga tarehe
ya 22 Juni, 1962, akazikwa Machui.
Alitunza kwa zawadi ya
waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa nishani
ya M.B.E.
Vitabu vyake
Maisha yangu
Kusadikika nchi iliyo angani
Kufikirika
Adili na nduguze
Masomo yenye adili
Utenzi wa Vita vya Uhuru
Wasifu wa Siti Binti Saad
Baada ya Miaka Hamsini
=======
2 comments:
Umetisha baab
Umetisha baab
Post a Comment