Shaaban Robert alizaliwa tarehe
1 Januari, 1909 kijiji cha Vibambani jirani na Machui kilomita 10 kusini mwa
mji wa Tanga, alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-salaam
kati ya miaka 1922 na 1926 alifaulu na kupata cheti.
Akaajiriwa na serikali ya
kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani mwaka 1926 – 1944.
Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa
mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu kumesaidia maendeleo yake
Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.
Tangu 1944 alihamia ofisi
nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mbali na maandio yake alikuwa
na athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa kamati
za East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na Tanganyika
Languages Board.
Kwa ujumla Mzee Shaaban Robert
aliandika vitabu ishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni: Adili na Nduguze,
Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad, Baada ya Miaka Hamsini, na
Maisha Yangu. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha za Kichina, Kiingereza na
Kirusi. Alifariki dunia tarere 22 Juni, 1962 na kuzikwa Machui. Aliacha wake
watatu na watoto kumi.
Wazazi wake wote wawili walikuwa
wa ukoo wa Mganga wa kabila la Kiyao. Hatujui sana habari za wazazi wake,
lakini twajua kwamba jina la baba yake halikuwa Robert. Jina hili ama latokana
na matamshi mabaya ya jina lake hasa au yawezekana kuwa ni jina alilopewa
alipokuwa skuli Msimbazi. Kwa muda mfupi yeye mwenyewe aliandika jina lake
‘Roberts’, lakini baadaye aliacha kuliandika hivyo. Alizaliwa Vibambani,
ambacho ni kijiji kilicho kusini ya Machui, yapata maili sita kusini ya Tanga,
tarehe mosi January mwaka wa 1909. Hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa
mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita Waswahili.
Kazi alizofanya alipokuwa
Karani wa Serikali:
Forodhani Pangani na mahali
pengine tokea mwaka 1926 mpaka 1944
Idara ya Wanyama tokea mwaka
1944 hata 1946
Afisi ya Mkuu wa Jimbo Tanga
tokea mwaka 1946 hata 1952
Afisi ya Kupima Nchi Tanga
tokea mwaka 1952 hata 1960.
Alipandishwa cheo kuwa Grade
III Higher Division mwaka 1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena kuwa
Grade II Local Service Alikuwa mwanachama wa East African Swahili Committee,
East African Literature Bureau, Tanganyika Languages, Tanga Township Authority
Alielemishwa Dar es Salaam toka
mwaka wa 1922 mpaka mwaka wa 1926, akawa mtu wa pili katika wanafunzi kumi na
mmoja waliofaulu mitihani yao na kupewa shahada ya kutoka chuoni, yaani School
Leaving Certificate. Alioa mara tatu: mke wa kwanza alikuwa Mdigo. Alikuwa na
watoto kumi. Alipofariki aliacha watoto watano. Pia aliacha dada yake (wa baba
mmoja) Mwana Saumu, na Mama Yake.
Marehemu akafariki Tanga tarehe
ya 22 Juni, 1962, akazikwa Machui.
Alitunza kwa zawadi ya
waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa
nishani ya M.B.E.
Vitabu vyake
Maisha yangu
Kusadikika nchi iliyo angani
Kufikirika
Adili na nduguze
Masomo yenye adili
Utenzi wa Vita vya Uhuru
Wasifu wa Siti Binti Saad
Baada ya Miaka Hamsini
0 comments:
Post a Comment