Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza juu ya umuhimu
wa kuongezwa nafasi za kazi kwa ajili ya kupunguza kiwango cha umasikini
barani Afrika. Ki-moonameyasema hayo kupitia ripoti iliyosambazwa hapo
jana na kusisitiza kuwa, kuongezwa nafasi za kazi ni moja ya njia muhimu
za kupunguza umasikini barani humo. Katika ripoti hiyo Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa amefafanua kuwa, barani Afrika kuna nchi kadhaa zenye
kiwango cha juu cha uchumi huku jamii nyingi ya nchi hizo ikiwa
inakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii, suala linalotokana na
kusahauliwa na serikali zao. Ameongeza kuwa, asilimia kubwa ya vijana
hawana ajira suala ambalo linatia wasiwasi mkubwa. Akizungumzia mpango
wa maendeleo wa baada ya mwaka 2015 kwa ajili ya kufikiwa malengo ya
milenia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, kuna haja kwa
nchi za Afrika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususan kwa vijana,
sanjari na kutokomeza udhoofu na badala yake kuweka miundombinu imara ya
kiuchumi katika nchi hizo.
0 comments:
Post a Comment