Robert Sylvester Kelly (amezaliwa tar. 8 Januari 1967) ni mwimbaji wa muziki wa R&B na soul-mtunzi wa nyimbo, rapa, na mtayarishaji wa rekodi kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama R. Kelly. Alianza kuingia katika kazi ya muziki kwa mara kwanza kunako mwaka wa 1992 akiwa na kundi la Public Announcement,
halafu baadaye Kelly akaenda kuwa kama msanii wa kujitegemea mnamo 1993
na kuweza kupata mafanikio makubwa kabisa kwa kazi za kujitegemea baada
ya kutoa albamu yake ya 12 Play.
Kelly alifahamika sana kwa mkusanyiko wa vibao vyake vikali kama vile "Bump n' Grind", "I Believe I Can Fly", "Gotham City", "Ignition", "If I Could Turn Back the Hands of Time", "The World's Greatest", na hip-hopera ya "Trapped in the Closet".
Kelly ameimba viitikio vya nyimbo kibao maarufu za hip-hop. Nyimbo ni pamoja na "Fuckin' You Tonight" ya The Notorious B.I.G., "We Thuggin'" ya Fat Joe, "Gigolo" ya Nick Cannon, na "Go Getta" ya Young Jeezy, na ameshirikiana na Jay-Z katika albamu mbili za pamoja.
Katika maisha yake binafsi, Kelly amekuwa na kashfa kadhaa za ngono. Taarifa zilielezwa kwamba amemwoa kabinti kadogo Aaliyah, ambaye yeye ndiye alikuwa mtunzi wake wa nyimbo. Kelly na Aaliyah wakasitisha ndoa yao. Baada ya kutolewa video ya mtu moja aliyedaiwa kuwa yeye kufanya mapenzi na msichana mdogo, Kelly akashtakiwa katika kesi kadhaa za ngono za watoto mnamo 2002. Baada ya makawio kadhaa, kesi yake ikapelekwa kizimbani mnamo 2008, na baraza la wazee wa mahakama likamwona Kelly hana kosa katika mshtaka yote 14.
album zake
- 12 Play (1993)
- R. Kelly (1995)
- R. (1998)
- TP-2.com (2000)
- Chocolate Factory (2003)
- Happy People/U Saved Me (2004)
- TP.3 Reloaded (2005)
- Double Up (2007)
- Untitled (2009)
show
- 2005: Trapped in the Closet (1–)
- 2007: Trapped in the Closet (13–)
- 2007: R. Kelly Live The Light It Up Tour
Tuzo
- American Music Award
- 2000: Favorite Male Soul/R&B Artist
- 2005: Favorite Male Soul/R&B Artist
- BET Awards
- 2003: Msanii Bora wa Kiume wa R&B
- BMI Awards
- 1998: Mwimbaji na Mtunzi Bora wa Pop wa Mwaka (kwa ajili ya “I Believe I can Fly”, “I Can’t Sleep Baby (If I)”, na “I Don’t Want To” (imerekodiwa na Toni Braxton)
- Grammy
- 1998: Wimbo Bora wa R&B ("I Believe I Can Fly")
- 1998: Mwimbaji Bora wa Kiume wa R&B ("I Believe I Can Fly")
- 1998: Wimbo Bora Halisi wa Kibwagizo cha Filamu ("I Believe I Can Fly")
- NAACP Image Awards
- 2001: Outstanding Male Artist
- 2001: Outstanding Music Video (“I Wish”)
- Soul Train Awards
- 1999: Best R&B/Soul Album, Male (R.)
- 1999: Sammy Davis Jr. Entertainer of the Year Award
- 2000: Best R&B/Soul or Rap Album (R.)
- 2001: Best R&B/Soul Single, Male (“I Wish”)
- 2001: Best R&B/Soul Album, Male (TP2.com)
- 2004: R&B/Soul Album, Male (“Chocolate Factory”)
- 2004: Quincy Jones Award for Outstanding Career Achievements
- 2006: Stevie Wonder Award for Outstanding Achievements in Song Writing
- Source Hip Hop Awards
- 1999: R&B Artist of the Year
- 2001: R&B Artist of the Year
- Vibe Awards
- 2003: R&B Vanguard Award
0 comments:
Post a Comment