Kutoka katika mkutano na waandishi wa habari, P Square
wamewaahidi watanzania onyesho la aina yake ambalo hawajawahi kuliona,
ambapo kwa mujibu wao wenyewe, watakamua jukwaani si kwa masaa mawili tu
kama ilivyokuwa imetangazwa awali, bali watatumbuiza mashabiki mpaka
watosheke kabisa.
Wasanii hawa wametoa shukurani za kutosha kwa East Africa Radio, East
Africa Television na wadhamini wengine kwa kufanikisha onyesho hili
ambalo litakuwa ni la kwanza kabisa baada ya wakali hawa kusherekea siku
yao ya kuzaliwa tarehe 18 mwezi huu.
Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa vipindi wa East Africa Radio
Bwana Nasser Kingu amewataka mashabiki kuwahi uwanjani katika burudani
hii ambayo amesema itaanza saa moja kamili usiku, siku ya kesho tarehe
23 Novemba ndani ya viwanja vya Leaders Club.
Kwa niaba ya wasanii kutoka hapa hapa nyumbani ambao wote walikuwepo
kuwakilisha katika mkutano na waandishi, Lady Jay Dee amewataka
watanzania kuhakikisha hawakosi burudani hii ya aina yake.
0 comments:
Post a Comment