Thursday, July 3, 2014

Arobaini ya marehemu 'Japanese' kufanyika kesho

Kisomo cha Arobaini ya aliyekuwa mwimbaji wa African Stars Revolution na baadae Double M Sound Amina Ngaluma 'Japanese' kinatarajiwa kufanyika kesho kwa wazazi wake, Kitunda Machimbo jijini Dar es Salaam.

Mume wa marehemu, Rashid Sumuni ameomba mashabiki na wadau wa muziki nchini kushirikiana katika Arobaini siku hiyo ambapo shughuli itaanza baada ya swala ya Alasiri na baadae kujumuika katika futari.
Ngaluma alifariki dunia Mei 15 mwaka huu kwa shinikizo la damu akiwa nchini Thailand ambako ndiko alikohamishia makazi yake kikazi akiwa na bendi ya Jambo Survivors na kuzikwa Mei 24 Jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...