Thursday, July 3, 2014

Rose Muhando akamata 'Pindo la Yesu'

Mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini Tanzania Rose Muhando anatarajia kuwashirikisha waimbaji nyota wa miondoko hiyo Afrika Mashariki katika uzinduzi wa albamu yake aliyoibatiza jina 'Kamata Pindo la Yesu'.

Gwiji huyo yupo katika mpango wa kuizindua albamu hiyo tarehe 3 mwezi Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo amegusia kuwa bado hajaweka hadharani orodha nzima ya waimbaji ambao watamsindikiza stejini japo kuwa ana mpango wa kumwalika mwanadada Anastazia Mukabwa kutoka nchini Kenya aliyeshirki katika wimbo wake Rose uitwao 'Kiatu Kivue'.
Rose Muhando ameelezea kuwa albamu yake hiyo mpya imesheheni nyimbo zikiwemo Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Kamata Pindo la Yesu, Facebook na nyinginezo nyingi.

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...