Waliokuwa wawakilishi wa bara la Afrika kwenye fainali za kombe la
dunia zinazoendelea nchini Brazil timu ya taifa ya Algeria, wamerejea
nyumbani na kupokewa kishujaa na mashabiki wa soka waliokuwa
wamejitokeza kwenye uwanja wa ndege wa mjini Algiers
Algeria wamerejea nyumbani, baada ya kutolewa kwenye fainali hizo
ambazo zinaingia kwenye hatua ya robo fainali, huku wakiweka rekodi ya
kufika kwa mara ya kwanza kwenye hatua ya 16 bora.
Mara baada ya kuwasili nyumbani wachezaji wa timu ya taifa ya Algeria
walipanda gari la wazi na kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa
Algiers kwa ajili ya kuwasalimu mashabiki ambao walijipanga pembezoni
mwa barabara kuwasubiri.
Hata hivyo mashabiki wengine walikwenda sambamba na gari hilo la wazi
kwa kutembea kwa mguu ikiwa ni kuonyesha ni vipi walivyopendezwa na
uwezo waliouonyesha wakati wakiwa nchini Brazil, kabla ya kutolewa na
Ujerumani kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora kwa kufungwa mabao mawili
kwa moja.http://www.dailymotion.com/video/x20obvn_arrivee-de-l-equipe-nationale-a-alger-apres-le-mondial-bresilien_sportFIFA wameizawadiwa timu ya taifa ya Algeria dola za kimarekani million 9
ambazo hutolewa kwa timu zote zilizofanikiwa kutinga kwenye hatua ya 16
bora.
0 comments:
Post a Comment